Nini kinatokea baada ya Papa kufariki?
Na RFI
KIFO cha Papa Francis, kimerejesha tena desturi za karne kadhaa ambazo zitapelekea kuchaguliwa kwa kiongozi mwingine wa kanisa hilo kupitia makadinali zaidi ya 100 ambao watakutana katika siku 15 zijazo.
Kwa sasa kanisa hilo linaingia katika kipindi kinachofahamika kama “sede vacante”, ambapo kadinali mwandamizi ambaye kwa sasa ni Kevin Farrell atachukua majukumu ya siku kwa siku hadi pale papa mpya atakapochaguliwa.
Ni kadinali pekee atakayesalia kwenye nafasi yake lakini wengine wote waliokuwa wameteuliwa na Papa watalazimika kujiuzulu.
Aidha makadinali toka duniani kotea watafanya vikao kadhaa na kuamua tarehe ya mazishi ambayo lazima iwe ni kati ya siku 4 hadi 5 tangu kifo chake na siku 9 za maombolezo.
Watangulizi wake wamezikwa katika kanisa la st Peters Basilica mjini Vatican, lakini mwenyewe alitaka azikwe katika kanisa la santa Maria Maggiore huko Roma, akivunja utamaduni wa awali ambao hata jeneza lake halitakuwa wazi kama ilivyofanyika kwa wengine.
Kipindi kingine kinafahamika kama “Papabili” baraza la siri la makadinali litakalokuwa na majukumu ya kuteua mrithi mpya, baraza hili litatenga tarehe ya uchaguzi ambayo lazima iwe kati ya siku 15 na si zaidi ya siku 20 tangu kifo chake.
Kwa sasa mfumo huu una makadinali 135 wapiga kura, 108 walichaguliwa na Papa Francis, ambapo 53 wanatoka Ulaya, 20 toka Amerika kaskazini, 18 toka Afrika, 23 toka Asia, wanne toka Ocenia na 17 toka Amerika Kusini.
Papa Francis alitambulika na wengi kama mtetezi wa watu wa chiniKura mbili hufanyika moja asubuhi na nyingine jioni hadi pale kadinali mmoja atakapopata theluthi mbili ya kura, moshi mweusi ukiashiria bado hajapatikana hadi pale moshi mweupe utakapotoka kuachiria kupatikana kwa Papa mpya.
Baada ya hapa, kiongozi wa makadinali ambaye kwa sasa ni Giovanni Battista, atamuuliza papa Mpya ikiwa anakubali uteuzi na jina gani angeoenda kutumia na kisha ya haya yote haraka sana atakuwa mchungaji wa Roma na Papa kwa wakati huo huo.
No comments