Header Ads

ad

Breaking News

Ridhiwani awataka Masheikh kuendelea kumuombe Rais Samia

Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Wenye Ulemavu. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakazi wa Msonga Chalinze wilayani Bagamoyo

Omary Mngindo, Msoga

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Wenye Ulemavu. Ridhiwani Kikwete, amewataka masheikh kuendelea kumuombea dua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ridhiwani ametoa rai hiyo kwenye hafla ya futari aliyoiandaa nyumbani kwake Msoga wilayani Bagamoyo, ambapo alisema ni vema kila sehemu yenye mikusanyiko inayohusu ibada, wasisahau kumuombea rais.

Alisema kuwa, Rais Samia ameituliza nchi, huku akieleza kwamba utulivu mkubwa unaoendelea nchini, tofauti na mataifa mbalimbali ambayo yana migogoro mikubwa.

"Watanzania tunapokutana tuendelee kumuombea sana kwa Mwenyezi Mungu amzidishie hekima mama yetu, ampe vipawa zaidi vya kuliongoza taifa leo kwa mafanikio makubwa sana," alisema Waziri Kikwete.

Aliongeza kwamba, "Lakini kupitia yeye, tunaomsaidia, Makamu wa Rais Dkt. Isdory Mpango, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na ndugu yetu upande wa pili Dkt. Hussein Ali Mwinyi, taifa letu linazidi kupiga hatua katika nyanja zote" alisema Waziri Kikwete.

Amebainisha kwamba, Dkt. Mwinyi ni msaada mkubwa kati ya Zanzibar na Bara, ndiyo maana Tanzania inazidi kuwa kinara wa amani barani Afrika.

"Naye ndugu yetu Hussein Mwinyi anatuhitaji sana kwenye dua, sababu kazi aliyonayo ya kuilea nchi siyo ndogo, unaweza kuona nchi kama nchi na uongozi ni uongozi, kwa hiyo kuombeana dua ni jambo la muhimu sana," aliongeza Waziri huyo.

Waziri Kikwete alitumia hafla hiyo kuwashukuru wana Chalinze kwa dua zao kwake ambazo zimekuwa msaada mkubwa katika kutimiza majukumu aliyopewa na Rais Samia.




No comments