Header Ads

ad

Breaking News

Kimeza atetea nafasi yake CCWT Bagamoyo

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Bagamoyo (CWT-Bagamoyo), Hamisi Kimeza akizungumza na walimu


Na Omary Mngindo, Bagamoyo
MWALIMU Hamisi Kimeza amechaguliwa tena kuendelea kukiongoza Chama cha Walimu Tanzania (CCWT) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Katika uchaguzi huo uliofanyika mjini Bagamoyo, Kimeza alishinda kwa kura 100 dhidi ya Alfred Ringi aliyepata kura 52, Bilal Mkeha 25, Johnes Nyamba 9 huku Linus Aidan akipata kura 7.

Nafasi ya mhazini ameshinda Siza Mnjokava (188), Samwel Mbwasi kura 6, wengine waliochaguliwa ni mwakilishi wa walimu Vijana David Phares (111) na mwakilishi shule za awali Stella Mwihambi (93).

Uwakilishi wa shule za msingi umekwenda kwa Elisante Kindulu (51), Beo Sumari (38), Msafiri Innocent (36) na Bahati Mohamed (32).

Katika uchaguzi huo nafasi mbili za wawakilishi wa shule za sekondari zimekwenda kwa Bernad Kapera na William Mrope.

Anna Choaji Mwakilishi kitengo cha walimu wanawake, mwakilishi wa walimu Phinus Tuarila, (walimu wenye ulemavu), Mzee Kihaku (Taasisi) na Beginus Mbiro (Vyuo).

Walimu wanawake Veronica Kirumbi (Mwenyekiti), Anna Choaji (Katibu), Theresia Kilimo (Mhazinj), wajumbe Hawa Magulumali, Pili Mrope, Teddy Setebe na Saida Msosa.

Wapiga kura katika mkutano huo ni mwalimu mmoja kutoka kila shule, chuo na ofisi ya elimu wilaya inayofahamika kama tawi la chama mahala pa kazi.

Wilaya ya Bagamoyo ina jumla ya walimu 2,189, kati yao wanachama wa CCWT ni 2,154 na matawi ya wawakilishi mahala pa kazi ni 195.


No comments