Header Ads

ad

Breaking News

DKT. Philip Mpango kuzindua mbio za Mwenge Aprili 2

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge (kushoto),  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John na Katibu Tawala Kassimu Mchata, wakikagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru

Na Omary Mngindo, Kibaha

MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, utakaofanyika Aprili 2, mwaka huu mkoani Pwani.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete alitoa kauli hiyo Machi 26, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano uliopo mjini Kibaha.

Waziri Kikwete alianza kumshukuru Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge kwa kazi kubwa inayoendelea katika kuelekea uzinduzi wa uwashwaji wa mwenge huo.

"Nielezee furaha yangu kwa namna kazi inavyoendelea vizuri, pia nitumie fursa hii kumshukuru Makamu wa Raia Dkt. Mpango kwa kukubali ombi letu la kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mbio za Mwenge," alisema Ridhiwani.

Katibu Tawala Kassimu Mchata alisema kila kitu kipo tayari huku akiongeza kwamba jukwaa kwa ajili ya mgeni rasmi linatarajiwa kuwasili Machi 29,2025.

Aliongeza kuwa vijana wa Alaiki wapatao 1,200 wanaendelea na maandalizi ya mwisho mwisho katika kuelekea uzinduzi huo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge alisema katika uzinduzi huo wananchi takribani 16,000 wanatarajiwa kushiriki sherehe hizo, huku akiongeza kwamba barabara zimeboreshwa tayari kuwapokea wageni kutoka mikoa mbalimbali.

"Tumeandaa eneo maalumu litakalowekwa magari ya viongozi kutoka mikoa mbalimbali, baada ya hapo kutakuwepo na magari maalumu yatayosafirisha wageni hao kutoka hapa kuelekea viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha (KEC), alimalizia Kunenge.

No comments