Mbunge Mavunde akabidhi mradi wa shamba wafanyabiashara wadogo Dodoma
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amekabidhi mradi wa shamba la zabibu kwa Wafanyabiashara Wanawake wa Masokoni (UWAWAMA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kongamano kubwa la wafanyabiashara wanawake wa masokoni lililoongozwa na Mwenyekiti wa UWT, Cde Mary Chatanda.
Makabidhiano hayo yalifanyika nana Februari 20, 2025 Mpunguzi, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanachama wa UWAWAMA.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kujenga na kuboresha miundombinu ya masoko jijini Dodoma, kazi ambayo imechochea kukua kwa biashara na kuongezeka kwa kipato kwa wafanyabiashara wadogo.
Mradi huu wa shamba la zabibu unategemewa kuongeza mapato na kutunisha mfuko wa wafanyabiashara wadogo.
"Ni imani yangu kwamba, mradi huu wa shamba utakuwa kichochea cha kukua kwa uchumi na mapato ya umoja na kuongeza tija kubwa katika biashara zenu, na nitahakikisha mnapata soko la uhakika wa mazao yenu."
Mradi huu ukawe nguzo kuu ya umoja,upendo na mshikamano na isiwe chanzo cha kupoteza umoja na kuruhusu mgawanyiko unaoweza kuleta athari kubwa ya ustawi wa umoja.
Naye, Mwenyekiti wa UWAWAMA, Anna James Mwita amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo anawajali kina mama na kuwainua kiuchumi.
Ameahidi kushirikiana kuutunza na kuuendeleza mradi huo ili ulete tija kwa kina mama wa masokoni sambamba na matumizi yenye tija ya fedha sh.10,000,000 wa lengo la kutunisha mfuko wa umoja.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akikabidhi fedha kwa viongozi wa Wafanyabiashara Wanawake wa Masokoni (UWAWAMA)Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akichukua chakula
No comments