Mapokezi ya Rais Dkt.Samia nchini Brazil
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Galeão Air Force Base Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil Novemba 16, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20.
Rais Dkt.Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe.Luiz InƔcio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini, kuchochea maendeleo endelevu na matumizi ya nishati mbadala.
No comments