KAMPUNI YA SARUJI YA MBEYA YAGAWA GAWIO KWA WANAHISA WAKE
Jambo la pili la kujivunia ni kampuni hii kuwa kampuni ya kwanza kumilikiwa na kuendeshwa na wazawa ikiwa ni uwezeshaji uliofanywa na serikali yetu.
Serikali kama mmoja wa wanahisa katika kampuni hiyo ikiwa na umiliki wa asilimia 25 na kupitia kwa Msajili wa Hazina imepokea kiasi cha sh. bilioni 3 na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wenye hisa asilimia 10 limepokea sh. bilioni 1.2 kama gawio.
Pia, ikumbukwe kwamba, umiliki wa hisa nyingi za asilimia 65 ndani ya Kampuni ya Saruji Mbeya, zilichukuliwa na makampuni ya Amsons ya Tanzania kutoka kwa Holcim ya Uswisi.
Hata hivyo, wanahisa walitembelea kiwanda cha kuzalisha saruji kilichopo Mbeya Mei 31,2024 na walisisitiza kuendelea kuunga mkono na kuhakikisha kuna ukuaji endelevu kwa miaka ijayo kwa faida ya wadau wote na kuongeza thamani kwa wanahisa wake.
Akizungumza na Wafanyakazi kiwandani hapo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alisema uwepo wa kiwanda hicho ni maono ya Mwalimu Nyerere miaka ya 1978, hivyo wanapaswa kuyalinda maono hayo kwa manufaa ya vizazi vyetu, lakini ili wafanye vizuri zaidi wanaitaji kupunguza gharama za uzalishaji ili kukuza faida yao.
Mbeya Cement Company Limited (MCCL)
ilianzishwa nchini Tanzania chini ya Sheria ya Makampuni, 2002 kama kampuni
binafsi iliyoko Songwe, Mbeya ambayo inajishughulisha na utengenezaji na uuzaji
wa saruji.
No comments