Header Ads

ad

Breaking News

Yanga yazinduka, yaichapa Villa Squad 3-2

 Haruna Shamte wa Villa Squad (kushoto) akijaribu kumzuia Keneth Asamoah wa Yanga;. Foto: Zuberi Mussa

MABINGWA  wa soka Tanzania Bara, Yanga, jana iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, dhidi ya Villa Squad katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Chamazi mjini Dar es Salaam.

Yanga walianza mchezo kwa kulisakama lango la Villa Squad, ambapo dakika ya kwanza, Shadrack Nsajigwa alipiga shuti kali lililotoka nje ya lango la wapinzani wao.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, walitawala mchezo dakika 10 za kwanza na kulifikia lango la wapinzani wao.

Dakika ya 11, beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', akiwa katika harakati za kuokoa kwa kichwa, mpira ulitua kwa Mohamed Kijuso aliyepiga shuti kali na kumgonga Nsa Job na kutinga wavuni.

Bao hilo liliizindua Yanga na kuifanya izidi mashambulizi, dakika ya 15, Haruna Niyonzima, aliisawazishia bao timu yake kwa mpira wa adhabu, baada ya kipa wa Villa kuchelewesha mpira na mwamuzi wa mchezo huo, Ibrahim Kidiwa kuamuru upigwe kuelekea langoni kwao.

Yanga ilipata nguvu baada ya kufunga bao hilo na kuliandama lango la Villa Squad, dakika ya 26, Keneth Asamoah aliiongezea timu yake bao la pili kwa kuunganisha mpira uliopigwa na Idrissa Rashid.

Hamis Kiiza aliyeingia badala ya Shamte Ally, aliwainua mashabiki wao baada ya kuifungia Yanga bao la tatu dakika ya 63, baada ya kuunganisha vizuri mpira wa krosi uliopigwa na Rashid.

Dakika ya 72, Kigi Luseke aliifungia Villa Squad bao la pili, kwa shuti kali lililompita kipa Yaw Berko.

No comments