Azam FC yailambisha koni Coastal Union
Coastal Union, jana walishindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani, baada ya kuchapwa bao 1-0, na Azam FC ya Dar es salaam, jana.
Azam FC walipata bao la kwanza kwa kichwa na John Bocco dakika ya 33, baada ya kupiga penalti mkwaju wa penalti uliopigwa na kutemwa na kipa Omari Hamis na mpira kutua kichwani kwake.
Penalti hiyo ilitokana na makosa ya beki wa Coastal Union, Said Swedi kumchezea vibaya Bocco.
Coastal Union walipata penalti dakika ya 67, baada ya said Morad wa Azam FC kumchezea vibaya Bernad Mwalala na mwamuzi Leonard Swai, kuamuru ipigwe penalti, lakini shuti la Sabri Mzee lilipanguliwa na kipa Mwadin Ally.
No comments