Header Ads

ad

Breaking News

Wana CCM Bagamoyo wachukua fomu kumrithi Sharifu


Na Omary Mngindo, Bagamoyo


WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamejitokeza kwa wingi kuchukua fomu ya kuwania Uenyekiti wa chama hicho wilayani hapa.

Hatua hiyo inakwenda kumpata Mwenyekiti atayeziba nafasi ya Abdul Sharifu ambae ametenguliwa na uongozi wa juu wa chama hicho chini ya rais Dkt Samia Suiuhu.

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kutamatika kwa zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu hizo, Katibu Mwenezi Ramadhani Lukanga alisema kuwa uchukuaji wa fomu ulianza Ijumaa na kutamatika Jumanne ya Jan 28.

Alisema kuwa wanachama 52 walichukua fomu za kuwania nafasi hiyo ambapo mpaka siku ya mwisho wa zoezi hilo wakirejesha wanaCCM 46 tu.

"Kwaniaba ya Kamati ya Siasa tunawapongeza wanachama waliochukua fomu, hatua iliyobaki ni kupanga tarehe ya kukaa kuanza kuyapitia majina, kabla ya kuyapeleka mkoani na ngazi ya Taifa kwa vikao vya mchujo," alisema Lukanga.

Aliongeza kwa kuwaomba wanaCCM wilayani hapa kutulia kusubili vikao vitavyoyapitia majina ya wagombea hao, kisha kurejeshwa hatimae uchaguzi ifanyike wa kumpata mrithi wa nafasi hiyo.

Aliongeza kuwa "Zoezi la uchukuaji wa fomu na mchakato wake wa uchujaji mpaka kupigwa kura kunakuwa na wanaCCM ambao wana wagombea wao, hivyo baada ya vikao na kupatikana kwa Mwenyekiti niwaombe tuvunje makundi tuendeleze umoja wetu," alisema Lukanga.

Uchaguzi wa Mwenyekiti unakwenda kuziba nafasi ya Abdul Sharifu aliyeongoza chama hicho kwa vipindi viwili, kabla ya maamuzi ya uongozi wa juu wa chama hicho kumuondoa kwenye nafasi hiyo.

No comments