Header Ads

ad

Breaking News

UINGEREZA YAVUTIWA NA MKAKATI WA TANZANIA KUONGEZA THAMANI MADINI NCHINI

*Waziri Mavunde asisitiza madini kuongezwa thamani ndani ya nchi

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akisisitiza jambo katika mkutano huo

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mh.Lord Collins amevutiwa na mpango wa nchi ya Tanzania kuandaa mkakati maalum wa uongezaji thamani madini nchini Tanzania na kuahidi kwamba Uingereza itatoa ushirikiano katika kusaidia eneo la uongezaji thamani madini hayo ndani ya nchi.

Hayo yamesemwa leo wakati wa kikao kati ya Mh. Lord Collins na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

“Tanzania na Uingereza zina ushirikiano wa muda mrefu katika maeneo mengi ya kiuchumi ikiwemo sekta ya Madini.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Lord Collins, akziungumza katika kikao hicho

Nimevutiwa na mkakati wa Tanzania wa kuongeza thamani ndani ya nchi, mkakati ambao Uingereza tunauunga mkono na tupo tayari kuwezesha utekelezaji wake kupitia Mradi wa “Manufacturing Africa“ ambapo ya pauni 2.1 bilioni zimetengwa  kusaidia nchi 6 za Afrika,ikiwemo Tanzania,kutengeneza bidhaa za kati na za mwisho kupitia madini“ Alisema Lord Collins.

Akizungumza katika Kikao hicho,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema Tanzania inayo mkakati wake maalum wa uongezwaji thamani madini ili kuongeza manufaa makubwa zaidi kwa nchi kupitia sekta ya madini,ambapo kwa sasa madini yanapaswa kuchakatwa na kuongezwa thamani nchini.

Serikali imetenga eneo maalum la ujenzi wa viwanda vyakuongeza thamani wilayani Kahama,Mkoani Shinyanga kwa lengo la kuvutia uwekezaji katika eneo hili.

Balozi wa Uingereza-Tanzania,  Marianne Young akizungumza katika mkutano huo

“Mradi wa “Manufacturing Africa“ utasaidia kufanikisha azma ya Tanzania kwa kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata,kusafisha na kutengeneza bidhaa zitokanazo na madini“ Alisema Mavunde.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Balozi wa Tanzania-Uingereza Mh. Mbelwa Kairuki na Balozi wa Uingereza-Tanzania Mh. Marianne Young.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akizungumza jijini Dar es Salaam
Waziri wa Madini Anthony Mavunde (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Lord Collins
Balozi wa Tanzania-Uingereza Mbelwa Kairuki (kushoto) na Balozi wa Uingereza-Tanzania,  Marianne Young wakijadiliana jambo
Waziri wa Madini Anthony Mavunde (kushoto)  na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Lord Collins, wakiagana baada ya kumaliza kikao

No comments