Dkt.Biteko: Chamwino msifanye makosa
*Amsifu Ndejembi utendaji kazi wake
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko akizungumza katika Mkutano Maalum wa CCM Jimbo la Chamwino uliofanyika wilayani Chamwino Februari 2,2025Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko amewataka wananchi wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma kuhakikisha hawafanyi makosa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Dkt.Biteko ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Chamwino wa Jimbo la Chamwino linaloongozwa na Mbunge Deogratius Ndejembi mbaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Makazi uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya wasichana ya Mkoa ya Manchari iliyopo Kata ya Manchali jimboni humo.
Amewapongeza wagombea walioteuliwa kuwania urais, Dkt.Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dkt.Emmanuel Nchimbi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, na Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuteuliwa kuwania nafasi ya urais kwa Zanzibar.
"Naomba tujipongeza wana CCM kwa kuteuwa watu wenye uweledi, uweledi wao usiotiliwa shaka, ni dhahiri kuwa ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi kutokana na uwepo wa wagombea hawa, ni ushindi ambao hautiliwa shaka kwasababu ya rekodi zao, uwezo wao na namna ambazo wanakijua ipi ni shida ya watanzania," anasema.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, aliwahoji wajumbe wa mkutano maalum wa Jimbo la Chamwino kama taarifa liyowasilisha na Mbunge wao Ndejembi kama wameipokea, ambapo kwa kali moa waliitikia, ndiyooo."
Mbunge wa jimbo hilo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 kwa wajumbe hao katika mkutano huo, ambapo aliwahoji mara tatu kama yote yaliyosomwa na mbunge wao yametekelezwa.
"Mbunge wenu Deo, sisi tuliyenaye bungeni, tunaomfahamu ni rafiki wa wengi, wabunge wooote wangepata nafasi ya kuja hapa, sikumbuki na wala sijawahi kusikia mbunge wa aina yeyote anayemsema Deo kama adui yake, Deo hana Jumatatu wala Jumapili, tabasamu kwake ndiyo sura na vazi lake wakati wote," amesema Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Niashati Dkt.Doto Biteko (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Chamwino na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius NdejembiAmeongeza kuwa, Deo anaweza kuwa na kasoro moja tu, kama haliwezekani atakwambia hili haliwezekani, Deo hakupotezei muda kukwambia maneno ya kukupaka sukari kwenye mdomo na Deo anajua kusema ndiyo penye ndiyo na hapana mahali ambapo pana hapana.
Amesema ni mbunge pamoja na mambo mengine, huwezi kuona anashughulika na watu, anashughulika na shida za watu wa Chamwino, Deo pamoja na umri wake mdogo wakati wote ni darasa kwa viongozi wengine mahali mbalimbali.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko (kushoto), akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deogratius Ndejembi wakati wa Mkutano Maalum wa CCM jimboni humo Februari 2,2025"Nataka kuwahakikishia wana Chamwino, wakati mmemchagua Deo na hata alipokuwa mkuu wa wilaya, mimi amesalia kuwa rafiki yangu kwa miaka mingi, ndiyo maana sikushangaa, Mheshimiwa Ndugai (Job), Spika mstaafu alipowaletea ushuhudu kwamba, Deo bado anakumbukwa hata Kongwa alipokuwa mkuu wa wilaya akifanya kazi," amesema.
Amesema ukimwona mtu anatajwa na mtu mahili, mbobezi wa siasa za nchi hii, tena kiongozi wa muda mrefu kama Job Ndugai, mtu yeyote anayetia shaka, mwambie pole kwa kuwa Ndugai amesema yeye ni nani asiunge mkono.
"Mheshimiwa Deo nataka kukuombea kwa Mwenyezi Mungu, mimi si kiongozi wa kiroho, lakini kwasababu huwa ninaomba ninataka kukuombea kwa Mwenyekiti Mungu aendelee kukupa afya njema, tumeshuhudia mapenzi ya wana Chamwino kwako," amesema.
Amesema kuwa, alipokuwa akizungumza, hakuona watu waliokuwa wakisimama simama na kutembea tembea, hivyo hakuona sababu ya kuwauliza kama watamchagua tena, kwani hao watu walishakubali kwa kuwaangalia machoni, na mwenyekiti wao wa CCM Mkoa alisema kanuni hazimruhusu kusema kuwa nani anafaa.
"Lakini mwenyekiti kanuni hizo hizo zinakutaka wewe kutafuta kiongozi anayefaa kwa ajili ya watu hao, kama unaona Ndejembi anafaa, wewe ni binadamu na kwa kweli tutashangaa kuona mwenyekiti asiyeweza kujua nani anayefaa, lakini amesema yeye mwenyewe miwshoni kuwa, kazi alizozifanya Ndejembi zinambeba," amesema.
Ameongeza kuwa, kwa wale waliosoma sehemu pengine, wanasema hata mwenyekiti amesema Deo anatosha.
Wana CCM wakisikiliza hotuba kutoka kwa viongozi walioshiriki Mkutano Maalum wa CCM Jimbo la Chamwino uliofanyika Kata ya ManchaliNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amewapongeza kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wana CCM Chamwino mmefanya uchaguzi mzuri wa amani, mmechagua viongozi a Chama Cha Mapinduzi, siri moja inachokifanya Chama Cha Mapinduzi kiendelee kubaki kwenye dola, zinaweza kuwa nyingi, lakini yeye anazijua chache mbazo ni Umoja na kufanya kazi kwa Pamoja.
"Mkiona vyama vingine vinapata ushindi katika uchaguzi, hawajipigii kura, tunawapigia wenyewe kwasababu tumegawanyika ndani yetu, niwaombe ana Chamwino, uchaguzi unaokuja siyo uchaguzi a majaribio, tunapaswa kuungana kwa Pamoja, tulivyo wengi tunaweza kuwa na tofauti mbalimbali, tunaweza kuwa na misimamo ya tofauti tofauti, ninawaombe tuache tofauti zetu, tukitazame chama chetu, tushikamane kwa Pamoja," amesema.
"Hatuna sababu ya kuhangaika kuwazungumza wengine, tuzungumzemambo tuliyonayo ndani ya chama chetu, nchi yetu ina vyama vingi vya siasa, vina kazi nyingi, chama kimoja kina kazi ya kufanya na vyama vingine vina maneno ya kusema, ninyi wana CCM fanyeni kazi, viacheni vyama vingine vibaki na maneno ya kusema, wananchi watawapima kwa kazi, hawatawapima kwa maneno mliyosema, wananchi watapima wakati huduma zinaimarika," amesema.
Ameongeza kuwa, "Wanajua wanasababu gani ya kuepeleka kura yao wapi, kuna wakati mwingine watani zenu watazungumza maneno ya kejeli, ndiyo maana kwenye mikutano yao hawawezi kumaliza bila ya kuitaja CCM, kwanini, kwasababu hawana ajenda wana maneno ya kusema na ni lazima waitaje CCm, kwasababu CCM ndiyo chama kiingozi, nyinyi wana Chamwino msiingie mtego huo kwa kukitaja hata chama kimoja, isipokuwa wale alioalikwa tu, kama ACT Wazalendo, watamtaja kama mgeni waliyemwalika," amesema.
"Shikamaneni, unganeni fanyeni kazi kwa Pamoja, kibebeni chama chenu wakati wote, kipiganieni na wakati wote kazi zilizofanywa na Chama Cha Mapinduzi isiwe siri ya kujua wawili watatu, semeni wakati wote na kila mtu aliye chama kingine mwonesheni upendo na kumvuta kuja kwenu," amesema.
"Nataka kuwakumbusha, mkiona chama cha siasi kimedondoka katika uchaguzi, ndani ya chama hicho watu wamegawanyika,tukatae magawanyiko ndani yetu, tuungane tubaki kuwa wamoja wana CCM na tuwaunge mkono viongozi wetu, Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa sana kwenye nchi yetu na mliona juzi wakati anatoa taarifa ya utekelezaji katika kipindi cha miaka michache hii, mabadiliko makubwa ameyafanya," amesema Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Amesema wana CCM wanao mfumo wa uongozi kuanzia ngazi ya shina, ngazi ya tawi, kwenye kata, kwenye wilaya mpaka ngazi ya taifa, watumieni mfumo wa uongozi wao, ambapo aliwataka mabalozi na viongozi wa mashina wasijione wadogo, wajione ni viongozi muhimu kwa ajili ya ushindi wa chama chao.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jimbo la Chamwino wakisikilizaAmeongeza kuwa, ushindi wa chama chao ndiyo nguvu yao wana CCM ya kuwafanya waendelee kufanya kazi ya kuleta maendeleo kwa watu wao.
Kuhusu kuwepo kwa hospitali ya wilaya, amesema jambo hilo amelichukuwa na mheshimiwa Ndejembi watashirikiana kwa Pamoja, na kwamba serikali inayoongozwa na Dkt.Samia ina mipango ya kujenga hospitali kila wilaya, hivyo watalishughulikia.
Amezungumzia suala la umeme, amesema sekta ya nishati chini ya Dkt.Samia iko salama, amemtoa wasiwasi mbunge kuwa, wana vitongoji 365 katika Wilaya ya Chamwino, hivyo wawape muda wanalifanyia kazi suala hilo.
"Mwaka jana Benki ya Dunia iliipima Tanzania kwenye upelekaji wa nishati ya umeme kwa wananchi, Tanzania iliongoza na ndiyo maana mkutano mkubwa wa viongozi nchibarani Afrika, umefanyika Tanzania siyo kwa bahati mbaya."
"Mpaka hivi leo wadau wa maendeleo mbalimbali duniani wamekubali na wameridhia kutoa fedha kwa ajili ya mpango wao kupeleka umeme kwa wananchi zaidi ya dola za Marekani bilioni 47, zimeshatolewa na wadau wa maendeleo ili tupeleke umeme kwa watu wetu," amesema.
Amesema ni suala la muda mfupi, kwani baada ya muda watahama kwani watakuwa wamemaliza nchi nzima vijiji vyote 12,318, na kuhamia kwenye vitongoji ambapo nchi nzima vipo 64,000, tayari wamepeleka vitongozi 32,000, wakati 33,000 vilivyosalia watapeleka umeme ili wananchi wahame kwen ye nishati isiyokuwa safi waende kwenye nishati iliyo safi.
Job Ndugai
Amewataka wana Chamwino kutofanya makosa wakati wa uchaguzi mkuu hapo baadaye, lakini aliwakumbusha kuwa, Deo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ambako alijifunza mambo mengi, hivyo wana Kongwa wanamhitaji akagombee ubunge kule.
Pamoja na maneno hayo ambayo alikuwa akiyatoa kama utani, lakini wana Chamwino walipiga kelele za kukataa mbunge wao akagombee Kongwa, kwani bado wanamhitaji, hivyo wasifanye makosa katika uchaguzi mkuu ujao.
"Hivi haya maendeleo mnayoyaona hata hapa tulipokaa, mliwahi kuona kumbi kubwa kama hizi hapa Chamwino, hapa tupo wachache nawaomba mpeleke salamu kwa haya tuliyoyasikia na mliyoyaona kwa wenzetu ambao hawakufika hapa," amesema Spika mstaafu Ndugai.
Wajumbe wa Mkutano Maalum Jimbo la Chamwino walikuwa na kauli mbiu yao, hivyo Mheshimiwa Ndugai alimalizia kwa kusema, Mama Samia, wao wakiitia mgombea wetu, Deo Ndejembi, chaguo letu.
Kibajaji
Wajumbe wa Mkutano Maalum wa CCM Jimbo la Chamwino wakisikilizaNaye, Mbunge wa ..Livingston Lusinde 'Kibajaji' amesema alikuwa akiangalia kanuni zinavyosema, angeweza kusema Mbunge Ndejembi apite moja kwa moja, lakini kanuni haziruhusu,hivyo amewataka wana Chamwino kuhakikisha wanamtendea haki mbunge wao wakati ukifika wa kupiga kura.
Amesema wagombea rasmi wa CCM ni Dkt.Samia na Nchimbi (Emmanuel Katibu Mkuu wa CCM), Naibu Waziri Mkuu pamoja na Deo ambao anaona kama wamepita moja kwa moja bila kupingwa, wakisubiri kuthibitishwa.
Anthony Mavunde
Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akizungumza katika Mkutano Maalum wa CCM Jimbo la Chamwino uliofanyika wilayani Chamwino Februari 2,2025Amesema wana Chamwino wana mbunge mwenye uwezo wa kusimamia na kuielendeleza Wilaya ya Chamwino na Jimbo la Chamwino.
Ameongeza kuwa, mheshimiwa Mbunge amepata nafasi ya kuteuliwa na kupewa heshima na mheshimiwa Rais kama Waziri, nafasi kubwa kabisa ambayo wanaamini wataendelea kumuenzi na kumpa ushirikiano mkubwa.
Amewaomba wana Chamwino kwamba, Deo bado ana nguvu za kutosha kuweza kuwatumikia kwa kujidhihirisha kwa maneno na vitendo kwamba ana uwezo wa kuwafanyia makubwa jimbo hilo, hivyo endeleeni kumpa ushirikiano ili aendelee kufanya kazi yake vizuri zaidi.
Amesema kuwa, Wilaya ya Chamwino imejaliwa kuwa na madini, wamefanikiwa kuzirejesha serikalini leseni 2,648 ambazo hazijafanyiwa kazi, ambapo Mbunge Ndejembi alimwomba mahsusi kwa ajili ya watu wa jimbo lake, hivyo wakianza utaratibu wa kutoa leseni wananchi wa jimbo la Chamwino watawakumbuka kuwapatia leseni.
Kuhusu mgogoro wa wananchi wa Haneti uliowasilishwa kwake, amemhakikishia Mbunge Ndejembi kwamba, wiki ijayo wataalam wa madini watakwenda na kifaa maalum kutambua mipaka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao bila usumbufu.
Mavunde amewakumbusha wana Chamwino kwamba, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu, ambapo Rais Dkt.Samia amefanya kazi kubwa anaamini watampa kura zote, pia Ndejembi anaamini watampa ushirikiano.
No comments