Header Ads

ad

Breaking News

Wenyeviti Kibaha Vijijini wapewa somo

Regina bieda, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya kibaha

Na Omary Mngindo, Mlandizi

WENYEVITI wapya ndani ya vijiji na vitongoji vinavyounda Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, wametakiwa kuwashirikisha wananchi katika shughuli za kimaendeleo.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Erasto Makala  katika hafla ya kuapishwa kwa wenyeviti hao, chini ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mlandizi Joseph Luoga, ambapo alisema hatua hiyo itawahamasisha kuithamini na kuilinda.

"Kwanza niwapongeze kwa kuchaguliwa hii inaonesha mnakubalika mbele ya wananchi, pesa nyingi zinaletwa kwenu niwaombe mkawashirikishe wananchi katika miradi, ili waone nao ni sehemu ya miradi," alisema Makala.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Hakimu Luoga, Mkurugenzi Mtendaji wa Regina Bieda aliwataka wenyeviti hao wakafanye kazi za wananchi, na kwamba nafasi zao ni sawa aliyonayo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Erasto Makala

"Serikali pamoja na Halmashauri inaelekeza fedha za miradi mingi katika maeneo yenu, nendeni mkazisimamie ipasavyo ili miradi inayowalengwa kwa wananchi wetu iweze kukamilika kwa viwango na wakati," alisema Bieda.

Aidha, Bieda amewataka Wenyeviti ambao hawakupata nafasi ya kuapishwa kutokana na sababu mbalimbali, wasianze kutekeleza majuku yao ya Uenyekiti mpaka atakapokamilisha zoezi hilo.

Akitoa neno kabla ya kuwaapisha, Hakimu Luoga alisema kuwa uwepo wao kama viongozi wa Seriki za mitaa, ni kwa mujibu wa Ibara ya 145 na 146 hivyo amewataka wazisome ibara hizo mbili.

"Msome Ibara hizo kwa sababu mnafanya kazi tatu, kama bunge kutokana na kutekeleza kanuni, kama Mahakama kuna migogoro mnaitatua, pia mnafanyakazi ya utawala kusaidia ulinzi na katika kila idara," alisema Mhe. Luoga.

Mkuu Idara ya Utumishi, Edward Masona
Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani, joel Kileo


No comments