Taasisi ya CSM yasaidia baskeli 300 Boko
Shukuru Lusanjala (Kushoto) Paulo Maguhwa (Katikati) na Josephine Gunda wa mbele wakijaribu baskeli hizo.
TAASISI ya Community Support Mission (CSM) chini ya Mwenyekiti Jonathan Mlokozi, imekabidhi baskeli 300 zenye thamani ya shilingi milioni 45 kwa wanafunzi wanaosoma shule za msingi na sekondari.
Baskeli hizo zimetolewa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kutoka Kata ya Boko, wanaosoma shule ndani ya kata hiyo na nje ya kata wanaotembea umbali mrefu kufuata elimu.
Akizungumza katika hafla ya kupokea baskeli hizo, Diwani wa kata hiyo Paulo Maguhwa alisema kuwa hatua hiyo inatokana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Taasisi Mlokozi aliyemwelezea changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.
"Kwanza nimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu kwa jitihada zake za kuboresha elimu, katani kwangu tumepata shule ya Sekondari pia namshukuru Mbunge Michael Mwakamo kwa kuendelea kutupambania," alisema Maguhwa.
Mwenyekiti Mlokozi alisema kuwa taasisi yake baada ya kupokea maombi hayo kutoka kwa Diwani huyo, aliwasiliana na wadau ambao wamefanikisha kupatikana kwa baskeli hizo, ambazo zitakabidhiwa kwa walengwa hao.
"Nilipokea ombi kutoka kwa Diwani Maguhwa kuhusiana na changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu wa kwenda na kurudi shule, nikawasiliana na Mdau leo hii tunakabidhi baakeli hizi," alisema Mwenyekiti huyo.
Mgeni rasmi Josephine Gunda Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Ruvu, aliishukuru uongozi wa CSM kwa kukubali ombi la diwani huyo, huku akiwaomba wanaBoko kutokusikiliza maneno ya wanasiasa.
"Diwani wenu amefanya jambo kubwa mfano wa kuigwa, hatua hii ni ya kupongezwa kwani inalenga kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu," alisema Gunda.
Shukuru Lusanjala akimwakilisha Mkurugenzi Regina Bieda alisema kuwa wameupoke msaada huo kwa furaha, unaolenga kuwaondolea kutembea umbali mrefu wanafunzi hao.
"Tunaushukuru uongozi wa taasisi kwa jitihada kubwa ambazo wamezionesha, Serikali tunathamini mchango wenu huu, unaounga mkono juhudi za Serikali yetu chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan," alisema Lusanjala.

No comments