Lion Club Host yakabidhi misaada ya shilingi milioni 1.6
Na Omary Mngindo, Chalinze
LION Club (Host) ya Dar es Salaam imewakabidhi watoto waishio katika mazingira magumu vifaa vya shule ikiwemo vyakula kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi Kijiji cha Kidogozero yenye shilingi milioni 1.6.
Vifaa hivyo ni madaftari, kwa wanafunzi 41 wa shule ya msingi na sekondari ambapo kila mmoja alipatiwa makaunta buku, mabegi na peni huku wa shule ya msingi wakikabidhiwa madaftari, peni na penseli sanjali na vyakula.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais mstaafu Muntazir Barwani alisema kuwa chama chao sio mara ya kwanza kufika Jimbo la Chalinze, na kwamba wamewahi kuchangia kuzawadia matenki manane katika shule za msingi na sekondari.
"Pia tulileta vifaa tiba katika Zahanati ya Ruvu Darajani sanjali na vifaa vya shule kwa wanafunzi, mwaka huu tumeona tuingie zaidi vijijini tumeleta Kidogozero kwa watoto wanaoishi mazingira hatarishi tumewapatia vifaa vya shule," alisema Barwani.
Mahmood Rajvani Rais wa chama hicho Dar es Salaam alielezea furaha ya kuwatembelea watoto hao, na kuwakabidhi vijana wa kikundi hicho misaada waliyonayo.
"Tulipokea taarifa ya kuwepo kwa kikundi hiki kinacholea watoto hawa, leo tumeluja kuwaona kisha kuwakabidhi vifaa vya shule sanjali na vyakula," alisema Rajvani.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Said Sango ameishukuru Lion huku akiongeza kwamba wakati Mohsin Barwani akiwa Diwani wa Kata amesaidia vitu mbalimbali ahuleni hapo, ikiwemo Kata kikiwemo matenki lililopo shule.
"Niwaombe wanafunzi mwende shule zitakapofunguliwa na wale wataoingia kidato cha kwanza sitegemei kubaki nyumbani, vifaa vya kuanzia mmepata kama hamna sare hata za nyumbani mwendenazo, kama mabegi mmeshapata," alisema Sango.
Akizungumza kwa niaba ya Diwani Mussa Gama, katibu wa diwani huyo Amos Mwakamale alisema kuwa hatua hiyo imeongeza faraja kwa wanafunzi hao, wakiwemo viongozi na kwamba anaimani kubwa kwamba vitawasaidia walengwa hao.
Zena Mindu Katibu wa kikundi cha Funguka Kidogozero alishukuru misaada hiyo, huku akieleza kwamba kikundi hicho chenye watoto 41 kimeshawahi kupokea misaada kutoka Lion huku akiuomba uongozi huo kutochoka kusaidia.
No comments