Header Ads

ad

Breaking News

WAZIRI DKT. GWAJIMA, BALOZI MPYA IRELAND WAZUNGUMZA


Na WMJJWM, Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Ireland nchini, Mhe. Nicola Brennan aliyetembelea ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam Septemba 12, 2024 kwa lengo la kujitambulisha.

Katika mazungumzo yao, Waziri Dkt. Gwajima amemweleza Balozi Nicola mafanikio, changamoto na maeneo ya kufanya kazi pamoja hususan eneo la jinsia.

Naye, Balozi Nicola amesema kuwa, eneo la jinsia ni kipaumbele hasa katika kuwawezesha wanawake kwenye maeneo ya vijijini kujikwamua kiuchumi.



No comments