WAKALA WA VIPIMO WAPATA MAFANIKIO, WATAKA USHIRIKIANO
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba 11, 2024 jijini Dar es Salaam
WAKALA wa Vipimo (WMA), amefanya mapinduzi makubwa ya huduma zake ili kumlinda mlaji na umma ikiwa ni matokeo ya uwezeshaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
WMA kazi yake kubwa ni kuhifadhi vipimo vyenye usahihi wa ngazi ya kati, kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika kwenye sekta za biashara, afya, usalama na mazingira.
Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla aliyasema hayo Dar es Salaam katika kikao kazi kati ya taasisi hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano inayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ili kuzipa nafasi taasisi na Mashirika yaliyo chini ya ofisi hiyo kuelezea majukumu waliyonayo, mafanikio na changamoto walizonazo.
Amesema mwaka wa Fedha 2025-2026, wanatarajia kutoa gawio la sh. bilioni 7.7 serikalini. Katika kipindi cha miaka wameendelea kutoa gawio ili kuhakikisha maendeleo yakapatikana kwa wananchi,wakati Mwaka wa Fedha 2018/2019 walitoa gawio la sh. bilioni 4.2. mwaka 2019/2020 sh. bilioni5.3. mwaka 2020/2021 sh. bilioni6.2. mwaka 2021/2022 sh. bilioni 4.2 na mwaka 2022/2023 walitoa gawio la sh. bilioni 4.3
Majukumu mengine ya WMA ni kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na vipimo kwa Serikali, Mashirika, taasisi na wadau wengine, kusimamia matumizi sahihi ya vipimo kwa njia ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.
Kuongezeka kwa idadi ya vipimo vinavyohakikiwa Kuendelea na Ununuzi wa vifaa vya Kitaalam pamoja na kuiwakilisha nchi kwenye masuala ya vipimo kikanda na kimataifa (AFRIMET, SADCMEL, EAMET, OIML).
WMA inatekeleza kwa vitendo maono ya Rais Dkt. Samia kwa kutoa huduma bora ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa nchi na mlaji, kuchangia katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
“Namshukuru sana Rais Dkt. Samia kwa maelekezo anayoyatoa kwetu ambayo yametusaidia kuboresha huduma tunazozitoa kwa ufanisi mkubwa,” amesema.
Kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali katika taasisi hiyo, mikakati waliyonayo ni kuendelea na ununuzi wa vifaa vya kitaaluma.
Mikakati mingine ni kuingia kwenye maeneo mapya ya uhakiki wa vipimo, kuendelea kutoa elimu kuhusiana na matakwa ya Sheria ya Vipimo, kuendelea kuboresha mifumo ya utendaji kazi, kujenga uwezo (Mafunzo, ununuzi wa vifaa).
WMA ni moja ya
Wakala za Serikali iliyoanzishwa Mei 13, 2002 kwa tangazo la Serikali namba 194
la Mei, 2002 ikitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vipimo, sura
namba 340. Awali WMA ilikuwa Idara, chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Afisa Mten Mkuu Bw. Alban Kihulla akionesha tuzo waliyopata kutokanana utendaji wao wa kanz. Kushoto ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw.Sabato Kosuri
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBbVUtW1Q6JpnoJ1hhqMzbW6_wBSci88UwVML3BqCRGpYhhI2M-JUHXUvqbzuH94UMvaquivBCrop8qRG99218mDtVvBLXBzhjqB83scI_X3fuBLTF7ukJpzjXRtcSSvFLNu_iL8Azhm1qHWlruMk97CegeEw9lm6Am3DlUrxrxaWTuBArKfOj4wU11dXE/w640-h436/PHOTO-2024-09-11-17-05-11.jpg)
Afisa Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw.Sabato Kosuri akifafanua jambo katika kikao kazi
No comments