Header Ads

ad

Breaking News

UADILIFU, UZALENDO VIWE NGUZO KATIKA UTENDAJI KAZI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI -WAKILI MPANJU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju

Na WMJJWM-Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju ametoa rai kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia uadilifu na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao nchini bila kukiuka sera na sheria zilizowekwa.

Ameyabainisha hayo katika Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Septemba 05,2024 linaloendelea Mkoani Dodoma.

Wakili Mpanju ameyaasa Mashirika hayo kuweka maslahi ya Taifa mbele ili kuweza kufikia malengo yaliyofikiwa kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

“Serikali ina jukumu la kuyawekea Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mazingira rafiki ili yaweze kutekeleza majukumu, hivyo mnapaswa kuzingatia mila na desturi za nchi yetu na kuweka uzalendo na uadilifu kwanza na kuachana na tamaa za fedha na kujikuta mnakubali mila zisizofaa,” amesema Mpanju.

Vilevile Wakili Mpanju ameyakumbusha mashirika hayo kuwa, yanayokiuka miiko, sera na sheria zilizowekwa basi yatachukiliwa hatua stahiki hivyo umakini unapaswa kuongezeka wanapoingia katika mikataba na wafadhili wa mashirika yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri kwa Rais juu ya masuala ya Kizazi chenye Usawa (GEF) Mhe. Angellah Kairuki ametoa rai kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwekeza jitihada za dhati, katika utekelezaji wa miradi itakayoweza kutatua changamoto zilizopo katika masuala ya Jinsia.

“Katika utekelezaji wa Miradi yenu inabidi muangalie kwa namna gani mnaweza kuelekeza programu zenu katika kutoa mafunzo kwa wanawake ili waweze kutumia Nishati Safi, wajengewe uwezo wa kushirki katika uongozi, kumilika ardhi na kushiriki katika kilimo lakini vilevile natoa rai muwekeze nguvu katika sekta ya afya hususani afya ya uzazi,” amesema Mhe. Kairuki.

Sambamba na hayo, viongozi wanne kutoka nchini Malawi akiwepo Katibu Mkuu wa Wizara pacha ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Ustawi wa Jamii na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka nchini Uganda wameshiriki Jukwaa hilo kwa mwaka 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri kwa Rais juu ya masuala ya Kizazi chenye Usawa (GEF) Mhe. Angellah Kairuki







No comments