Siza apeta ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Vijijini mkoani Pwani, Hamisi Bigo
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani (Kibaha Vijijini), mwishoni mwa wiki wamemchagua Siza Lyimo kuwa Mjumbe wa kuwakilisha Taifa kupitia chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu Mwenezi wa chama hicho wilayani hapa Hamisi Bigo alisema kuwa katika uchaguzi huo wanaCCM zaidi ya 12 walijiyosa kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Tunamshukuru Mwenyeezimungu tunefanikiwa kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi moja iliyoachwa Humoud Jumaa, ambae kwa sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (CCM) kupitia Jumuia ya Wazazi Taifa," alisema Bigo.
Aliongeza kuwa kwa sasa wana CCM hao wanawakilishwa na Mkali Kanusu, Abdallah Macho, Mbunge Michael Mwakamo na Siza Lyimo ambao watakuwa na jukumu la kuwasemea katika ngazi za Taifa ndani ya chama hicho.
Kwa upande wake Mohamed Chawawa alisema kuwa katika uchaguzi huo wanaCCM walitumia Demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa ambapo Siza Lyimo amechaguliwa kuahika nafasi hiyo.
" Uchaguzi ulikuwa huru na haki, ambapo Siza ndio mshindi kwemye kinyang'anyiro hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Pentagon uliopo Mlandizi katika stendi Kuu ya Mlandizi," alisema Chawawa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Siza alielezea furaha yake kwa wanaCCM hao kuona yeye anatisha kuwawalilisha katika Mkutano Mkuu wa chama hicho Taifa, na kwamba ameahidi hatowaangusha.
"Kwanza nimpongeze Rais Dkt. Samia Suluhu kwa namna gani anayoiongoza nchi yetu, pia niwashukuru wanaCCM wenzangu chini ya Mwenyekiti shupavu Mkali Kanusu kwa kazi kubwa anayoiendeleza ya kutuongoza wanachama wake," alimalizia Lyimo.

No comments