Simba Nguvu Moja Mlandizi latapa viongozi
Mwenyekiti mpya wa tawi la Mlandizi (Simba Nguvu Moja), Senkondo Msuya
Na Omary Mngindo
WANACHAMA wa Simba tawi la Mlandizi (Simba Nguvu Moja) limepata vuongozi wataoliongoza kwa kipindi cha miaka minne ijayo.Uchaguzi huo uliohudhuliwa na wana Simba 62, umefanyika baada ya kumalizika kwa uongozi wa muda uliokuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti Senkondo Msuya, aliyeongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Katika uchguzi huo uliofanyika kwenye tawi la klabu hiyo, nafasi ya uenyekiti ilikuwa ikigombewa na wanachama wawili ambao ni Nassoro Shomvi (Mbilinyi) na mtetezi wa nafasi hiyo Senkondo Msuya huku Mbilinyi akiibuka mshindi.
Makamu Mwenyekiti Mawazo Baruti na Katibu Heri Achahofu wote walikosa wapinzani, Katibu Msaidizi Fatuma Yussufu, wakati Abdallah Tengeneza 'Dege la Pori' akishinda nafasi ya usemaji kwa kumbwaga Mohamed Kipilale.
Akitangaza matokeo hayo, Jafari Mohamed (Msua) aliyekuwa Mwenyekiti wa uchaguzi alisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, na wagombea ambao kura zao hazikutosha walikubali matokeo hayo.
Wajumbe Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Salum Kindema, Salma Mpembenwe, Zakia Ibrahimu, Ally Kawambwa, Abdallah Zungo, Mawazo Sadiki, Robert Edward, Juma Mwinyimvua na Mintanga Sinahabari.
Akizungumza baada ya kukamilisha uchaguzi huo, Mbilinyi aliwashukuru wanachama hao kwa kuwachagua viongozi hao, huku akieleza kwamba kwa umoja wao wataendeleza pale walipoishia waliomaliza muda.
"Kwa niaba ya viongozi wenzangu tuliochaguliwa leo tunawashukuru wanachama kwa kuonesha imani yao kwetu, tunawaahidi hatutawaangusha tutafanyakazi ipasavyo," alisema Mbilinyi.
No comments