Header Ads

ad

Breaking News

Sekondari ya Pera yapiga hodi benki ya NMB Chalinze

Diwani wa Kata ya Pera Jackson Mkango akitoa neno

Na Omary Mngindo, Chalinze

UONGOZI wa Shule ya Sekondari ya Pera iliyopo Kitongoji cha Pingo Kata ya Pera umepiga hodi katika Benki ya NMB tawi la Chalinze, ikiomba iiwekee mfumo wa gesi, umeme na maji kwenye jiko shuleni hapo.

Hayo yameelezwa na Mwalimu Mkuu Alex Kamaga mbele ya mgeni rasmi Mbaruku Nyenga ambaye ni meneja wa benki hiyo, hatua inayolenga kupatikana kwa nishati mbadala.

"Ndugu mgeni rasmi shule yetu pamoja kupatikana kwa mafanikio lukuki ikiwemo ya vyumba vipya vya madarasa, walimu na ufaulu mzuri tunaiomba Ofisi yako ituwezesha kupata mfumo wa gesi, umeme na maji ili tuondokane na matumizi ya kuni," iloeleza sehemu ya taarifa.

Aliongeza kuwa zoezi hilo linataraji kugharimu zaidi ya shilingi milioni 12, hatua itayoiondolea shule matumizi ya kuni, huku ikiunga mkono juhudi za Serikali kutunza mazingira.

Akijibia risala hiyo, Nyenga alisema kuwa NMB ni mdau mkubwa wa Serikali katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo, huku akiutaka uongozi huo kuandika barua itayoainisha upatikanaji wa vifaa hivyo.

"Benki ya NMB imekuwa mdau mkubwa wa Serikali katika kuunga mkono juhudi za maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, nikuombe Mwalimu andikeni barua ipitie maeneo huaika jisha nilileteeni nitaiwasilisha kwa viongozi wa juu," alisema Nyenga.

Diwani wa Kata ya Pera Jackson Mkango alisema kuwa kazi kubwa imefanyika ya ujenzi wa vyumba vipya vya Madarasa, ikiwemo barabara inayoingia shupeni hapo huku akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu na Mbunge Ridhiwani Kikwete.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Pera Kaisi Chombo amewashukuru walimu, huku akiwaomba wazazi na walezi kuwaunga mkono katika kazi zao.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Pingo Idi Fuko alisema kuwa akiwa mjumbe wa Serikali miaka 20 iliyopita alishiriki kutengwa kwa eka 50 zilizotumika kujengwa shule hiyo na Zahanati, huku akisema kuwa kuna baadhi ya watu wanamchukia kwa tamaa zao za kutaka kuuza sehemu ya ardhi hiyo.

Mwalimu Mkuu Sekondari ya Pera Alex Kamaga (shuti bluu) akimkabidhi taarifa mgeni rasmi Mbaruku Nyenga, Meneja wa Benki yaNMB tawi la Chalinze, katiia mahafali ya nne shuleni hapo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Pera Kaisi Chombo akitoa neno. Picha zote na Omary Mngindo.

No comments