Header Ads

ad

Breaking News

MBUNGE UMMY AFUNGUA MAFUNZO YA UMOJA WA VIJANA CCM TANGA MJINI

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 8/9/2024 amefungua mafunzo ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Tanga chini ya mwenyekiti wake Ndugu Ismaili Samangago.

Katika ufunguzi huo, Mhe Ummy alisema kuwa Tanga Mjini tuna kila sababu kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri za maendeleo anazofanya  hasa jambo kubwa la Upanuzi wa Bandari ya Tanga na sasa tunaona matunda yake kwa kuongeza fursa za biashara, ajira na uwekezaji kwa watu wa Tanga.

Mhe Ummy pia ametumia nafasi hiyo kuwahimiza vijana  kugombea katika nafasi za uchaguzi wa serikali za Mitaa, nafasi za Udiwani na Ubunge kwa kuwa tumeshakubaliana nafasi ya Uraisi ni ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pekee. Mhe Ummy alisema kuwa CCM inabebwa na Wanawake na Vijana hivyo ni muhimu pia vijana kuwa sehemu ya maamuzi kwa kuwa kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 Vijana wa umri wa miaka 15 hadi 35 ni takribani asilimia 34 ya watanzania wote.

Aidha Mhe amekubali maombi  ya UVCCM Wilaya ya Tanga ya kununua simu 8 kwa ajili ya kuongeza nguvu za usajili wa kadi za eletronik kwa umoja wa vijana na sare 500 za Vijana wa Hamasa.

Semina hiyo ya mafunzo imehudhuriwa na Wajumbe wa Baraza la UVCCM Wilaya ya Tanga, Waheshimiwa madiwani na Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Tanga ndg Salim Kipanga .

No comments