JWTZ yaishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge Ushelisheli
Na Omary Mngindo
MNADHIMU Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Zanzibar (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Othuman, ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje Kisiwa cha Ushelisheli.
Shukrani hizo zimetolewa na Luteni Jenerali Othuman, akizungumza na Kamati hiyo iliyotembelea Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma Sept 3, ambapo alielezea kufurahishwa kwake kwa kutambuliwa mchango mkubwa uliotolewa na jeshi hilo.
"Niishukuru Kamati yenu kwa kuuona, kuutambua na kuuthmini mchango mkubwa ambao jeshi letu umeutoa katika harakati za ukombozi wa Bara letu la Afrika," alisema Luteni Jenerali Othuman.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Francois Adelaide alisema kuwa, JWTZ limekuwa msaada mkubwa kwa nchi nyingi za Kusini mwa Bara la Afrika.
Aliongeza kwamba nchi yake itaendelea kukuza Diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi na kubadilishana ujuzi, kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kudhibiti majanga.
"Tutaendelea kukuza Diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi ikiwemo kubadilishana ujuzi kukabilina na uharifu unaovuka mipaka, pamoja na kudhibiti majanga," alisema Makamu Mwenyekiti hiyo.
No comments