Header Ads

ad

Breaking News

Jumaa awataka wanamichezo kuchukua fomu

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuia ya Wazazi Humoud Jumaa

Na Omary Mngindo, Ruvu

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuia ya Wazazi Humoud Jumaa, amewataka wanamichezo kuchukua fomu za uongozi ili wamuunge mkono Rais Dkt. Samia Suluhu.

Jumaa alitoa rai hiyo akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa, ambapo alisema kuwa Tanzania imempata Rais anayependa michezo hivyo ni fursa kwa wanaMichezo kujitokeza kuwania uongozi nafasi mbalimbali.

Alisema kuwa Rais Samia ni mwanamichezo namba moja, ukweli unaodhihirishwa na kuongeza hamasa kwa vilabu vya Yanga, Simba, timu ya Taifa na vingine zinavyopeperusha bendera ya nchi.

"Nitumie nafasi hii kuwaomba wanaMichezo nchini kujitokeza kuchukua fomu za nafasi za uongozi, ili kuunga mkono juhudi za Rais wetu kipenzi anayejitoa katika kuendekeza michezo," alisema Jumaa.

Aliongeza kwamba kupitia hamasa yake ya kununua kila goli maarufu "Goli la Mama" limekuwa chachu kubwa kwa vilabu vinavyowakilisha nchi kwenye michuano mbalimbali ya Kimataifa.

"Tunazishuhudia vilabu vya Yanga, Simba na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Star's) zinazofanya vizuri katika michuano inayoahiriki, msimu iliomalizika tumeishuhudia Yanga ambayo kama si figisu ilikuwa imetinga fainali," alisema MNEC huyo.

Alisema kwamba ameshuhudiwa akipiga simu moja kwa moja viwanjani kuzitakia heri vilabu vya Yanga ba Simba, ukweli unaoshihirishwa ni namna gani anavyopenda michezo.

Aliongeza kwamba "Kwa ukweli huo kuna kila sababu kwa wanamichezo kuchukua fomu za kuwania uongozi, ili pamoja na masuala mengine pia wsaidie Rais katika kuendeleza michezo," alisema Jumaa.

No comments