Header Ads

ad

Breaking News

ZANZIBAR REGGAE FESTIVAL KUFANYIKA 9-10 AGOSTI 2024


Na Andrew Chale, Zanzibar


TAMASHA kubwa la muziki wa Rege (Reggae) Zanzibar msimu wa Sita linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia usiku wa Ijumaa Agosti 9-10, 2024, Mambo Club ndani ya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.

Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Said Omary Hamad 'Side Rasta' Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha wasanii na utayari wa tamasha hilo, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano, huku akiomba wadau kujitokeza kudhamini kwani ni moja ya matamasha yanayoongeza fursa za kiuchumi visiwani humo.

Side Rasta amesema Zanzibar Reggae Festival ni moja ya matamasha makubwa Afrika Mashariki kwa sasa hivyo, ni wakati wa makampuni binafsi na taasisi za kiserikali kujitokeza kudhamini tamasha hilo.

"Muziki wa Rege unahamasisha amani na umoja na upendo.

Ni muziki wenye ustaarabu na kuponya pia hivyo hii ni fursa ya kipekee kwa wadau kujitokeza kudhamini ili kuongeza tija kwa vijana na maendeleo katika nchi.

Side Rasta amesema Kenya wameweza kuupa nguvu muziki wa rege hivyo, ni wakati sasa kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kulikimbilia Ttmasha hilo ili liweze kuimarisha uchumi.

Aidha, amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kwani wasanii wote wamefika na maandalizi yote yamekamilika.

Aidha, amewatambulisha baadhi ya wasanii watakaopanda jukwaani ni pamoja na Mani Kifimbo (Bagamoyo Tanzania Bara), msanii kutoka Rwanda, 2T Reggae Man, msanii kutoka Kenya Mwanadada Salma Queen, msanii kutoka Kenya Jamaica, Nat Sterling.

Pia, wapo msanii mkongwe wa rege, Ras Gwandumi kutoka Tanzania Bara, KUSHITE, Ras Coco (Zanzibar),| KOM ZOT na wengine wengi.

Baadhi ya wasanii hao akiwemo Ras Gwandumi, 2T, Salma Queen, Nat Sterling kwa upande wao wameahidi kufanya onesho kubwa na la aina yake.

No comments