WIZARA TATU ZAJADILI HALI YA UZALISHAJI CHUMVI NCHINI
DODOMA
WIZARA ya Madini kwa kushirikiana na Wizara ya Mipango na Uwekezaji pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara zimekutana kujadili namna ya kuondoa changamoto katika sekta ndogo ya chumvi nchini.Wizara hizo zimekutana leo Agosti 15 , 2024 jijini Dodoma kufuatia taarifa zilizowasilishwa kwa Serikali na Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA) kuhusu changamoto zinazoikabili sekta hiyo ndogo ya chumvi ikiwemo kudorora kwa biashara ya chumvi hapa nchini.
Kikao hicho kilijumuisha Waziri wa Viwanda na Biashara *Dkt. Suleiman Jaffo* ,Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji *Mh. Prof. Kitila Mkumbo* na Waziri wa Madini *Mh. Anthony Mavunde* pamoja na Wadau wa Chumvi Nchini.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa,Wizara ya Madini kupitia *STAMICO* imewahakikishia wadau juu ya ufungwaji wa kiwanda cha kusindika Chumvi katika Wilaya ya Kilwa,Mkoa wa Lindi kabla ya
Mwisho wa Mwezi Desemba 2024.
No comments