Wanafunzi wa shule tano waweka kambi Msoga
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani, Miriam Kihiyo akizungumza mbele ya Hassani Mwinyikondo
WANAFUNZI wa shule tano za msingi na moja ya sekondari ndani ya Kata ya Msoga wameanza kambi maalumu ya kujiandaa na mitihani yao inayotaraji kufanyika hivi karibuni.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata hiyo, Hassani Mwinyikondo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi ya kata, kabla ya kumkabidhi vyakula hivyo ofisa elimu msingi Miriamu Kihiyo, hatua inayolenga kuwawezesha kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayoielekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu ambayo katika awamu ya sita imekuwa ikiendelea kufanya vizuri zaidi.
"Nimeunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha wanafunzi wanakaa kambi itayowawezesha kufanya vizuri kwenye mitihani yao," alisema Mwinyikondo.
Aidha Mwinyikondo alisema kuwa "Pia namshukuru Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete (Waziri wa Nch Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na wenye Ulemavu) ambae amekuwa msaada mkubwa katika kusukuma jimbo katika sekta mbalimbali," alisema Mwenyekiti huyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Kihiyo alimpongeza Mwinyikondo kwa msaada alioutoa wa mchele, unga, mihogo na nyanya utaosaidia kwa kiwango kikubwa katika kifanikisha zoezi hilo.
"Pia namshukuru Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete kwa kazi kubwa anayoendelea kuwatumikia wanaChalinze, tunashuhudia mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali," alisema Kihiyo.
Mtoro Tamla, Abdul Tengwe Mwalimu Mkuu shule ya Changa walishukuru kwa msaada huo, huku Omary Kisina Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Msoga akieleza kwamba msaada huo sio wa kisiasa, bali unalenga kuendelea elimu.

No comments