WANACCM Kibwende waingiwa na hofu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Mlandizi, Livinus Cleophace akizungumza na wana CCM
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kata ya Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, wameingiwa na hofu, baada ya moja ya shina lao kugomea vikao.
Mgomo huo unaofanywa na Shina namba tano katika Kitongoji cha Kibwende unatokana na wana CCM hao kutosikilizwa kilio chao kinachohusiana na mazao yao kuliwa na ng'ombe huku wakikosa msaada.
Mmoja wa wajumbe wa shina la wanaCCM hao Zainab Magimba, mbele ya Mwenyekiti wa Jumuia ya Vijana ya chama hicho (UVCCM) Kata hiyo Livinus Cleophace alisema kuwa wanashina hao namba 4 wanafanya hivyo ikiwa ni kushinikiza kusikilizwa kwa madai yao.
"Wale wenzetu wanamsikiliza sana Katibu wao anachokisema ndio huchohichomara, kadhaa wanasunbukiwa na mifugo kwenye mashamba yao eneo la Mto Ruvu, inapotokea mifugo kula mazao basi woote wanatelemka huko kwenda kupambana na wafugaji," alisema Magimba.
Aliongeza kwamba "Taarifa hizo zilimfikia Mwenyekiti wa Kitongoji pamoja na Mbunge, lakini wanasema kwamba mpaka sasa hakuna hatua ambazo zimeshachukuliwa hali inayowawafanya wasusie vikao vinavyoitishwa," alisema Magimba.
Tumaini Msuya Mjumbe wa shina Frem tano aligusia kero ya kukosekana kwa umeme katika baadhi ya eneo la Kibwende, nae Alid Chiwanga akionesha kushangazwa kwa kusuasua huko huku akisema kwamba mradi huo ni wa REA.
"Nikuombe Mwenyekiti katika majumuisho fanyeni mpango Mbunge Michae Mwakamo awepo ili atolee ufafanuzi, ikiwezekana aitishe mkutano azungumze na wananchi," alisema Chiwanga.
Akizungumza na wanaCCM hao tawi hilo, Cleophace alizungumzia mgomo uliofanywa na qanachama wenzao, ambapo alisema kuna haja kubwa ya kukutana nao ili kuzungumza hatimae kumaliza kero yao.
"Wale ni wenzetu haiwezekani tuwaache tu, nitafikisha taarifa hiyo kwa viongozi wa Wilaya ili tuone ni namna gani tunavyoweza kumaliza ili tatizo," alisema Cleophace.
Zainab Magimba akitoa ufafanuzi kwenye kikao hicho
No comments