Header Ads

ad

Breaking News

TANAPA YAPOKEA MAGARI 13 KUTOKA FRANKFURT

Na Philipo Hassan - Arusha

Kamishna wa Uhifadhi, Mussa Nassoro Kuji -  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo 07/08/2024 amepokea jumla ya magari 13 yaliyofanyiwa matengenezo na Shirika la kimataifa linalojihusisha na Uhifadhi, Frankfurt Zoological Society (FZS) chini ya mradi wa Emmergency and Recovery Support for Biodiversity (ERSB).

Akizungumza katika hafla ya  makabidhiano hayo iliyofanyika katika ofisi za FZS, Arusha, Kamishna Kuji alisema “magari tuliyoyapata yataelekezwa  katika shughuli za uhifadhi na utalii ili kuleta tija katika ulinzi wa maliasili zilizomo katika Hifadhi za Taifa“

Aidha, Kamishna Kuji alitoa wito kwa FZS kuendelea kuongeza  wigo zaidi katika kuendeleza juhudi za uhifadhi ili kusaidia jamii kubwa ya watanzania.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa  Shirika  la Frunkfurt Zoological Society (FZS), Dkt.  Ezekiel Dembe alieleza kuwa TANAPA inashirikiana vizuri na Shirika hilo katika kuendeleza uhifadhi na kwamba magari waliyoyatengeneza yatagawanywa katika Hifadhi za Taifa zaidi ya kumi (10) ili kuendeleza shughuli za uhifadhi.
 

Hifadhi za Taifa zitakazonufaika ni pamoja na Burigi-chato, Mto Ugalla, Ibanda-kyerwa, Kisiwa cha Rubondo, Milima ya Mahale, Rumanyika-Karagwe, Mkomazi, Serengeti, Ziwa Manyara na Katavi.

Magari hayo 13 yalichukukuliwa mwaka jana na FZS kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti yakiwa mabovu na kuanza kuyatengeneza kwa kutumia mafundi wa ndani.

 Shirika  la Frunkfurt Zoological Society (FZS) limekuwa na mchango mkubwa kwa kuonyesha jitihada katika uhifadhi wa maliasili  hapa nchini ikiwemo kusaidia miradi mbalimbali inayojumuisha jamii na uhifadhi.




No comments