Header Ads

ad

Breaking News

MAN KIFIMBO, 2T,SALMA QUEEN WAFANYA KWELI ZANZIBAR REGGAE FESTIVAL 2024

Na Andrew Chale, Zanzibar.

WASANII wa muziki wa Reggae Man Kifimbo (Tanzani), 2T Reggae Man (Rwanda), Salma Queen (Kenya) na msanii Nast Sterling (Jamaica) wamekonga nyoyo za wapenzi wa muziki huo kwenye msimu wa sita wa Zanzibar Reggae Festival 2024, katika viunga vya Ngome Kongwe, Mambo Club, Agosti 9,2024.

Wasanii hao kwa nyakati tofauti walilishambulia jukwaa kwa nyimbo zao mbalimbali zenye ujumbe mzuri na kuwaburudisha mashabiki wa muziki waliohudhuria onesho hilo.

Awali, msanii Man Kifimbo alifungua pazia la mwaka huu kwa kupiga nyimbo zake za Nipe Tano, Nunu, Sema basi, Money Money Pesa, Usikate miti, Usinga na nyingine nyingi huku msanii 2T akiwakonga nyoyo mashabiki kwa nyimbo zake kama, Fasha, Champion Woman na nyingine nyingi.

Wasanii Salma Queen, aliburudisha kwa nyimbo zake zikiwemo Two face, People Rise na Mama Africa, huku msanii Nat Sterling alishusha kupitia nyimbo zake kali za Rasta shine na nyingine.

Aidha, usiku wa Agosti 10,2024, msanii mkongwe wa reggae, Ras Gwandumi kutoka Tanzania Bara, Ras Coco (Zanzibar), Kushite, Kom Zot wanatarajia kufunga tamasha hilo kwa shoo ya aina yake.






No comments