Kiwangwa kumchukulia fomu ya Ubunge Ridhiwani
Malota Kwaga akiteta jamb na mmoja wa wanachama wa CCM Kata ya Kiwangwa, huku Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Ridhiwani Kikwete akisikiliza.
Kauli ya wanachama hao imetolewa mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho ngazi ya Kata, ulioandaliwa na Diwani Malota Kwaga ambapo alisema kuwa azimio hilo limetolewa katika moja ya vikao vya chama hicho.
Mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana Ajira na wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa jimbo hilo, Kwaga alisema kuwa hatua hiyo inatokana na kazi kubwa inayoendelea kutekelezwa na mbunge wao ndani ya Kata na jimbo kwa ujumla.
"Mheshimiwa Waziri tunamshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu kwa kazi kubwa ya kuwatumikia waTanzania pia kuonesha imani kwako, nasisi tunakupongeza kwa namna unavyodhihirisha kuwa ni mchakapakazi," alisema Kwaga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hassani Mwinyikondo alisema kuwa maendeleo ya Chalinze yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na Ridhiwani, kwani yeye ndio anayechukua changamoto zao kisha kumpelekea Rais Samia.
"Msione vinaelea mjue vimeundwa na muundaji wetu kwa Chalinze ni Ridhiwani Kikwete, kwetu katika nafasi ya ubunge tumefunga mjadala hatutaraji kumuona mwanaCCM yeyote atayechukua fomu, mbunge wetu ni Ridhiwani," alisema Mwinyikondo.
Akizungumza na wanaCCM hao, Ridhiwani alisema kuwa kuonekana kwake kwa Rais Samia kumechangiwa na wanaChalinze waliomchagua kushika nafasi hiyo, na kwamba rais asingemuona kama asingekuwa Mbunge.
"Rais Dkt. Samia Suluhu ameniona na kuniteua katika nafasi hii kutokana na nyie wanaChalinze kunichagua kuwa Mbunge wenu ndio rais akaniona, nawahakikishia kwamba nitaendelea kuipeperusha vizuri bendera ya wanaChalinze," alisema Ridhiwani.
Na Omary Mngindo, Kiwangwa
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kiwangwa, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, wameahidi kumchukulia fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge, Mbunge wao Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.Kauli ya wanachama hao imetolewa mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho ngazi ya Kata, ulioandaliwa na Diwani Malota Kwaga ambapo alisema kuwa azimio hilo limetolewa katika moja ya vikao vya chama hicho.

No comments