Header Ads

ad

Breaking News

KASEKENYA AIAGIZA TANROADS, WANANCHI KULINDA BARABARA

 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo alipokagua ukarabati na ujenzi wa barabara ya Kilwa na Mkuranga-Kisiju yenye urefu wa  kilometa 45 mkoani Pwani

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amezungumzia umuhimu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), kushirikiana na wananchi kulinda hifadhi za barabara na hivyo, kuwezesha ujenzi wa miundombinu hiyo kufanyika kwa urahisi na kudumu kwa muda mrefu.

Akikagua ujenzi wa barabara ya Mkuranga-Kisiju yenye urefu wa kilometa 45 na barabara ya Kilwa mkoani Pwani, amehimiza ushirikishwaji wa wananchi katika kulinda hifadhi ya barabara ili kuepuka uvamizi wa hifadhi hizo na usasababisha uchimbaji wa mchanga na mawe, hivyo kuathiri barabara na madaraja wakati wa mvua.

" TANROADS waelimisheni wananchi ili wazuie wenzao kulima, kujenga na kuchunga mifugo kwenye hifadhi za barabara ili kulinda barabara na kuzikarabati kwa urahisi inapohitajika," amelekeza Kasekenya.

Mkoa wa Pwani ni mkoa wa viwanda hivyo ujenzi na ukarabati wa barabara za Kilwa na Mkuranga-Kisiju kilometa 45 uzingatie ubora na viwango vya juu ili kuwezesha magari makubwa kusafirisha malighafi na bidhaa za viwandani kwa urahisi wakati wote.

"Kukamilika kwa barabara ya Mkuranga -Kisiju kutaongeza tija kwenye Bandari ya Kisiju na hivyo kuvutia wawekezaji wa hiwanda na hoteli," amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali iko katika hatua za mwisho kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kufanya ukarabati mkubwa kwenye maeneo yote ya barabara na madaraja yaliyoathiriwa sehemu kubwa na mvua zilizonyesha mwaka huu.

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Mhandisi Zilli Kihoko amesema watahakikisha hifadhi za barabara, maeneo ya maegesho na madaraja yanalindwa ili yadumu na kuleta tija kwa wananchi.

















No comments