Header Ads

ad

Breaking News

Jumaa ataka Dkt.Samia aungwe mkono

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC), kupitia ya Jumuia ya Wazazi, Humoud Abuu Jumaa


Na Omary Mngindo, Mlandizi
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC), kupitia ya Jumuia ya Wazazi Humoud Abuu Jumaa, amewataka waTanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu, kwani anafanyakazi kubwa.

Jumaa ametoa rai hiyo Julai 30 akizungumza na Majira mjini hapa, ambapo alisema kuwa Rais Samia anafanyakazi kubwa katika kila sekta, zinazoendea kuwapunguzia kama si kuzimaliza changamoto zinazowahusu wananchi.

Alisema kuwa ukweli wa kazi hiyo unathibitishwa na ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, barabara, maji, afya, umeme sanjali na ununuzi wa magari ya kubeba wagonjwa yakiwemo ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

"Katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu umekuwa na mafanikio makubwa kwa waTanzania, ametuondolea michango tuliyokuwa tunachangishwa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kila mwaka, ambayo Serikali imechukua jukumu hilo," alisema Jumaa.

Alisema kuwa katika sekta ya afya Rais amenunua magari zaidi ya 500 yaliyosambazwa katika Zahabati, Vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya kubeba wagonjwa, hatua inayolenga kuhakikisha waTanzania wanaendelea kupata huduma bora ya afya.

"Pasipokusahau sekta ya maji, mbali ya kuboreshwa kwa usambazaji wa huduma kupitia DAWASA na RUWASA pia Dkt. Samia amenunua mitambo ya kuchimba visima katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na miundombinu ya maji ya taasisi hizo," alisema Jumaa.

Aliwaomba waTanzania kutambua kazi kubwa inayoendelea kutekelezwa na Rais Samia, kwa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa daftari la kudumu, pia kupiga kura za kuchagua viongozi kuanzia Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

"Hatuna budi kumpongeza rais wetu kwani amefanyakazi ambayo awali hakuna aliyedhani kama anaweza kuitekeleza, lakini amekuwa jasiri na ameonesha ni namna gani wanawake wanavyoweza kusimama imaea katika uongozi," alimalizia Jumaa.




No comments