Header Ads

ad

Breaking News

DAWASA waeleza mafanikio na changamoto zao, wamshukuru Dkt.Samia

 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire akizungumza katika kikao kazi cha taasisi hiyo, wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo Jumatano Agosti 7,2024 jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), limekutana na wahariri na waandishi wa habari na kueleza mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 Akizungumza katika kikao kazi hicho kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, ameelezea mafanikio ya taasisi muhimu.

 Amesema DAWASA imefanya maboresho mbalimbali yenye lengo la kuleta ufanisi wa kuhudumia wateja, ambapo wamepata mafanikio makubwa katika uzalishaji na uanzishaji wa miradi mipya.

Amesema kwasasa uzalishaji wa maji kwa DAWASA umeongezeka kutoka lita milioni 520 kwa siku hadi lita milioni 534.6 kwa siku, sawa na ongezeko la lita milioni 14.6 kwa siku.

 Amesema mbali na kuongezeka kwa uzalishaji maji, pia uwezo wao wa kuifadhi maji umeongezeka kutoka lita milioni 154 hadi lita milioni 184 sawa na ongezeko la lita milioni 30.

 Ameongeza kuwa, mtandao wa usafirishaji na usambazaji maji nao umeongezeka kutoka kilomita 4,690.7 hadi kufikia kilomita 7,087, wakati ule wa majitaka uliokuwa wa kilometa 450 kwasasa umefikia kilometa 517.12, sawa na ongezeko la kilometa 67.12, ambapo wateja waliounganishwa majisafi wameongezeka kutoka 343,019 hadi 438,177.

 Pamoja na mafanikio hayo, Mhandisi Bwire amesema DAWASA wana changamoto ingawa wanapambana nazo kuzitatua. Changomoto mojawapo ni ile ya uvamizi na uharibifu wa vyanzo vya maji, mabadiliko ya tabia nchi, elimu kwa wananchi na ujenzi wa bwawa la Kidunda.

Ameitaja nyingine ni Changamoto ujenzi wa makazi usiozingatia taratibu za mipango miji, ushirikiano na wadau (Tanroads, Manispaa) katika kutatua changamoto na uvamizi katika maeneo ya hifadhi ya miundombinu ya maji.

 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema kwamba, changamotyo nyingine ni uchakavu wa mabomba na upotevu wa maji zinachangia kurudisha nyuma juhudi za taasisi.

 Amesema wanaendelea mpango wa kutoa elimu kwa wananchi ya umuhimu wa kulipia huduma ya maji wanayopata, kwani fedha hizo ndizo zinazosaidia kutatua mambo mengi ya kiuendeshaji.

Kuhusu miradi mipya, Mhandisi Bwire amesema miradi mipya inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na mradi wa maji Dar es Salaam ya Kusini, uliosainiwa Oktoba 31, 2023, ambao ni ujenzi wa tanki la ujazo lita milioni 9, wenye thamani ya sh.bilioni 34.5.


Afisa Uhusiano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafiri wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wahariri na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 7,2024 jijini Dar es Salaam.

 

Kabla ya kuanza kwa kikao kazi hicho, Afisa Habari Mwandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, amewakumbusha wahariri na waandishi wa habari umuhimu wa vikao kazi hivyo, huku akiwataka kuzingatia yale yote yatakayowasilishwa.

“Ninawaomba haya yatakayozungumza kwenye kikao kazi hizi yazingatieni, yatawasaidia katika kazi zenu,” amesema.

 Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tazania (TEF), Deodatus Balile, walishukuru DAWASA kwa kuwasilisha wasilisho hilo lililokuwa na mambo meingi muhimu ambayo mengine yalikuwa hayajulikana.

 Balile amesema mafanikio makubwa, aliyoyataja Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, yanatokana na utendaji mzuri wa kazi wa watendaji wot echini ya Mhandisi Bwire.

Ameongeza kuwa, DAWASA wanatakiwa kupambana kumaliza kero zilizopo ili kuongeza ufanisi wa taasisi katika kuwahudumia wananchi, lakini akimtaka kuwaondoa watendaji ambao hawataki kutekeleza majukumu yao.

 Mwenyekiti wa TEF amesema wanatamani DAWASA wakamilishe kazi ya kufunga mita za maji kila nyumbani yenye huduma ya maji, akiamini kwamba itasaidia kujua sehemu ambayo maji yanapopotelea.


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire akizungumza katika kikao kazi 


Afisa Uhusiano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafiri wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wahariri na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 7,2024 jijini Dar es Salaam.

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Bi. Everlasting Lyaro akizungumza katika kikao kazi














No comments