Header Ads

ad

Breaking News

BALOZI NCHIMBI APOKEA TAARIFA UTEKELEZAJI ILANI MCHINGA, AMPONGEZA MBUNGE MAMA SALMA KIKWETE KWA KAZI NZURI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi, akizungumza katika mkutano uliofanyika jimboni Mchinga mkoani Lindi
Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Mhe. Salma Rashid Kikwete akizungumza katika mkutano uliofanyika jimboni kwake


Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi, amesema ameisikiliza kwa makini taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Mama Salma Kikwete na viongozi wenzake kwa kazi kubwa waliyoifanya.

"Niseme nimeisikiliza taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, tena kwa umakini sana kwa niaba ya CCM nakupongeza wewe na viongozi wenzako kwa kazi kubwa unayofanya. Umetembelea kata zote na vijiji vyote. Umetumia hadi bodaboda na bajaji kuwafikia wananchi wa Jimbo la Mchinga, unaguswa na changamoto za wananchi wenzako wa Mchinga na unapambana kutatua kero zao kwa kuzisemea Bungeni na kuwaomba mawaziri kufika huku wao wenyewe.”

“Wakati wa natazama ile video ya uwasilishaji wa taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani, kuna mama mmoja amesema hakutegemea kwa hadhi yako ulivyo, kwamba ungeweza kulizunguka jimbo zima la Mchinga. Mimi pamoja na wenzangu wajumbe wa sekretarieti tumefurahishwa sana ya utekelezaji huu mzuri wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2020/2025, ndani ya miaka hii mitatu. Tunakutakia kila la heri katika kumalizia hayo mengine yaliyobakia katika kukamilisha Ilani ya 2020 - 2025.”

Naye, Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Salma Rashid Kikwete wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2025, amepongeza Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye nchi yetu ya Tanzania, pamoja na Jimbo la Mchinga, ambapo hadi sasa ambapo takriban Sh. 18.4 bilioni zimetumika katika Sekta ya Elimu ikiwemo kujengwa Shule ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi Mchepuo wa Sayansi, iliyojengwa katika Kijiji cha Kilangala huku uboreshaji wa huduma za afya ukifanyika kwa mafanikio makubwa na umeme tayari umefika katika vijiji vyote jimbo zima, sasa unaanza kuunganishwa kwenye vitongoji.

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Mama Salma Kikwete amekabidhi pikipiki kwa Polisi Jamii wa Jimbo la Mchinga na shule za sekondari katika kata zote za jimbo hilo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi (kushoto), akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Mheshimiwa Salma Rashid Kikwete, wakati wa mkutano uliofanyika Mchinga mkoani Lindi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi (kulia), akisalimiana Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jimboni Mchinga mkoani Lindi


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), akisalimiana na 
Mbunge wa Jimbo la Mchinga ambaye pia ni mke wake, Mhe. Salma Rashid Kikwete












No comments