Header Ads

ad

Breaking News

Wenye ulemavu wa ngozi Chalinze wahitaji mliioni 25


Na Omary Mngindo, Msoga


WATU wenye ulemavu wa ngozi katika Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 25, zitazowawezesha kununua ardhi, kujenga ofisi na usafiri wa bodaboda.

Hatua hiyo inalenga kufanikisha uboreshaji wa uwapatiaji huduma kwa walengwa hao wanaoishi pembeni mwa miji, ikiwemo kuwapatia elimu jamii yenye imani potofu inayohusiana na watu hao.

Hayo yamebainishwa na Christine Mdumuka, Mhasibu wa taasisi hiyo ambapo alisema kuwa, hatua hiyo inalenga kuwajengea uwezo wa kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwake ya kuwafikia wenzao wanaoshi pembeni mwa mji.

"Taasisi yetu ya TAS tumeianzisha watano, lengo la ombi la pesa kiwango hicho ni tununue kiwanja, tujenga ofisi na kununua pikipiki ili tuifikie jamii kuwapata elimu ya kuwaondo na dhana potofu ya kwamba, viungo vyetu vinawapatia utajili," alisema Mdumuka.

Steven Thomas, Katibu wa taasisi alisema hawana ofisi maalumu na kwamba, wamepanga chumba kwa ajili ya ofisi, huku wakilabiliwa na changamoto za kifedha hivyo wanawaomba wadau akiwemo Mbunge Ridhiwani Kikwete.

"Tuna kiu kubwa ya kuwafikia wenzetu wanaoishi pembezoni mwa mji wetu ambao kwa kiwqngo likubwa ndio wanaokumbana na changamoto kubwa inayohusiana na hali zetuu, tunamuomba Mbunge Ridhiwani, Madiwani na watu mbalimbali kutuunga mkono," alisema Thomas.

John Stephano mjumbe alielezea masikitiko yako yanayotokana na vitendo vya kishirikina vinavyofanyika katika jamii, huku akielezea kusikitishwa kwake na mauaji yanayoendelea yakihusisha jamii yenye Ualbino.

"Tunaiomba Serikali na jamii kuendelea kukemea vikali tabia inayoendelea dhidi yetu ya ukatili haswa katika kipindi kama hiki cha kuelekea kwenye chaguzi mbalimbali, hali inatisha sana," alisema Stephano.

Fatuma Athumani aliiba Serikali liendelea litoa adhabu kali kwa watu wanaobainika kutenda ukatili kwa watu wenye ulemavu hususani wa ngozi.



No comments