WAZIRI UMMY MWALIMU AMWAKILISHA RAIS SAMIA NCHINI ETHIOPIA
Na WAF, Ethiopia
WAZIRI wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewasilisha rasmi ujumbe maalum wa Rais Dkt Samia kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Ethiopia Mheshimiwa Sahle-Work Zewde, Julai 8,2024.
Waziri Ummy pamoja na wajumbe wake amekabidhi rasmi ujumbe maalum kwa Mheshimiwa Sahle - Work Zewde, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ethiopia jijini Addis Ababa Ethiopia.
Akipokea salaam hizo, Rais wa Ethiopia aliishukuru Tanzania kwa ushirikiano mzuri Katika nyanja mbalimbali ambao ulianzishwa na waasisi wa mataifa haya mawili
Kwa upande wake Waziri Ummy amemshukuru Rais Sahle - Work Zewde kwa kutenga muda wake na kupokea ujumbe maalum wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments