Wagonjwa 15 kuzibuliwa mishipa ya damu ya moyo iliyoziba kwa asilimia 99
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani
wakimfanyia mgonjwa upasuaji mgumu wa kuzibua mishipa ya damu iliyokuwa imeziba
kwa asilimia 99 na kushindwa kupitisha damu vizuri kwa kutumia tundu dogo
wakati wa kambi maalumu ya siku saba inayofanywa na wataalamu hao katika
taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Maalumu
Wagonjwa 15 ambao mishipa
yao ya damu ya moyo ilikuwa imeziba kwa asilimia 99 na kushindwa kupitisha damu
vizuri kufanyiwa upasuaj wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa
Cathlab.
Aidha wagonjwa wengine 10 ambao valvu
zao za moyo zilikuwa zimeziba nao watafanyiwa upasuaji wa kufungua valvu hizo
kupitia tundu dogo lililopo kwenye paja.
Upasuaji hizo zinafanyika katika
kambi maalumu ya siku saba inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika
lililopo nchini Marekani.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hii daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Kawajika Mwinyipembe alisema wapo baadhi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji
katika kambi hiyo matibabu yao hayakufanyika hapo awali kutokana na ukosefu wa
baadhi ya vifaa.
“Kwakushirikiana na wataalamu kutoka
Shirika la Madaktari Afrika tumeweza kupata vifaa vya kisasa vya matibabu vinavyotumika
kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba kwa asilimia 99 kuwasaidia wagonjwa
wetu lakini pia kuweza kubadilishana uzoefu”, alisema Dkt. Mwinyipembe.
Dkt. Mwinyipembe alisema wagonjwa
ambao valvu zao za moyo zimeziba mara nyingi ufanyiwa upasuaji wa kufungua
kifua lakini kutokana na teknolojia kukua wagonjwa hao siku hizi ufanyiwa
upasuaji kupitia tundu dogo.
“Tunatarajia kuzibua vavlu zilizoziba
kwa asilimia 99 kwa wagonjwa 10 bila ya kuwafanya upasuaji wa kufunga kifua,
matibabu ambayo yatamsaidia mgonjwa kupona kwa haraka na kutumia muda mfupi
hospitali tofauti na mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo,” alisema
Dkt. Mwinyipembe.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa
upasuaji mdogo wa moyo kutoka Shirika la Madaktari Afrika Joanna Ghobrial
alisema wataalamu kutoka Shirika la Madaktari Afrika wamekuwa wakishirikiana na
wataalamu wa JKCI lengo likiwa kubadilishana uzoefu na kuwasaidia wagonjwa
wanaohitaji matibabu ya moyo.
Dkt. Joanna alisema wataalamu wa JKCI
wameendelea katika kutoa huduma za upasuaji wa moyo wa aina mbalimbali utaalamu
ambao huko mbeleni hawatahitaji wataalamu wa mashirika makubwa kuwasimamia
katika kutoa huduma za upasuaji wa moyo.
“Madaktari Afrika tumekuwa
tukishirikiana na Taasisi hii kwa muda mrefu na matokeo ya ushirikiano wetu
tunayaona, hapo baadaye wataalamu wa JKCI hawatatuitaji tena kwani
wameshabobea,” alisema Dkt. Joanna.
No comments