Header Ads

ad

Breaking News

Vijiji 151 vimebaki nchi nzima kupata huduma ya umeme - Kapinga


Na Mwandishi wetu, Njombe

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema vijiji 151 tu nchi nzima ndio ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme kati ya vijiji zaidi ya 12,000 ambapo wilayani Ludewa mkoani Njombe vimebaki vijiji nane.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo jana tarehe 19 Julai 2024 wakati wa ziara ya kikazi katika vijiji vya Lubonde na Maweni wilayani Ludewa mkoani Njombe akikagua miradi ya nishati.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kapinga alifanikisha kuingiwa makubaliano kati ya Kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya Madope iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya kukabidhi miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme kwa Shirika hilo baada ya kusainiwa kwa mkataba kati ya pande hizo mbili.

Mhe. Kapinga amesema kuwa Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na Kanisa Katoliki kwa kushirikiana na Serikali kwenye uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Njombe, Eusebio Kyando ameupongezi Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano wao na kutoa fedha zilizowezesha kufanikisha mradi huo.

Kampuni ya Madope ni miongoni mwa wazalishaji wadogo wa umeme katika Wilaya ya Ludewa ambayo inamilikiwa kwa asilimia 55 na Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe.









No comments