Header Ads

ad

Breaking News

UCSAF YATUMIA SHILINGI BILIONI 2.16 YA KUJENGA MINARA 22 MKOANI SHINYANGA


Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Shinyanga


Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 2.16, kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano, kujenga minara 22 ya mawasiliano mkoani Shinyanga.

Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Bi Justina Mashiba amesema, minara hiyo imejengwa katika halmashauri tano za mkoa huo, kwa teknolojia ya 2G, 3G na 4G, na itawanufaisha watu zaidi ya 319,897.

Bi. Mashiba amemweleza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb.), aliyepo katika ziara ya kikazi mkoani Shinyanga kwamba minara hiyo imejengwa katika Wilaya za Kahama Manispaa, Kishapu, Msalala, Shinyanga DC na Ushetu.

Kuhusu mradi wa mnara 758 inayojengwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara, Bi. Mashiba amesema Mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa hiyo, inakojengwa minara 30, na ruzuku ya UCSAF iliyotumika ni Shilingi Bilioni 4.27.

Amesema hadi kufikia mwishoni mwa Juni 2024, minara 9 imekwishawashwa, na baadhi ya kata ambazo vijiji vyake vimenufaika ni Bokomela, Idahina, Lunguya, Mwalugulu, Mwanase, Busangwa, Shagihilu, Lyamidati na Solwa.

Mtendaji Mkuu huyo wa UCSAF amesema hadi sasa, minara iliyokwishawashwa katika mradi huo wa minara 758 itakayowanufaisha watu milioni 8.5 itakapokamilika ni 186.

Akitoa ripoti kwa Waziri Nape kuhusu Mnara uliojengwa na Kampuni ya Halotel Mwakilishi wa kampuni hiyo, amesema tangu uwashwe Mei 27 mwaka huu tayari watu 200 wameanza kutumia simu huku wengine wakiendelea kuuziwa simu janja na kampuni hiyo kwa mkopo.

Mwakilishi huyo wa Halotel amesema wamelenga kuendelea kukopesha na kuuza simu na laini ili kuwafikia wakazi zaidi ya 4,400 watu wazima wa vijiji vinavyohudumiwa na mnara huo wa 2G na 3G.




No comments