Header Ads

ad

Breaking News

TAWA YAITUMIA SABASABA KUTOA FURSA ZA UWEKEZAJI

 
Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Beatus Maganja

Na Batus Maganja, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania kuwekeza katika maeneo inayoyasimamia.

TAWA imeamua kuyatumia maonesho ya 48 ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam kuhamasisha wafanyabiashara wazawa na wageni kutoka mataifa mbalimbali kufanya uwekezaji wenye tija.

Akizungumza na watu waliotembelea banda la TAWA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, Afisa Utalii Daud Tesha amesema TAWA ina uwanda mpana wa fursa za uwekezaji unaotoa mwanya kwa wawekezaji wa aina mbalimbali kuwekeza katika mamlaka hiyo.

Tesha aliyataja maeneo yanayofaa kwa uwekezaji kuwa ni maeneo ya utalii wa picha kwenye maeneo ya hifadhi za Wanyamapori, maeneo ya kihistoria yenye Utalii wa kiutamaduni, eneo la uwekezaji mahiri (Special Wildlife Investment Concession Areas - SWICA), Uwindaji wa Kitalii na Ufugaji wa Wanyamapori

"TAWA imetenga maeneo kadhaa kwa ajili ya kufanya shughuli za utalii wa picha kutokana na ikolojia na aina ya vivutio vilivyopo katika maeneo hayo ikiwemo Pori la Akiba Mpanga/Kipengere eneo ambalo lina maporomoko ya maji zaidi ya 10 ambayo hutoa burudani safi kwa watalii," amesema Daud Tesha.

"Maeneo mengine ni Pori la Akiba Wamimbiki, Tabora ZOO, Ruhila ZOO , Makuyuni Wildlife Park ambapo wananchi wanakaribishwa kuwekeza kwenye miundombinu ya Utalii ikiwemo kujenga kambi za kulala wageni (Campsites), hosteli, loji na maeneo ya mapumziko mafupi kwa watalii (Picnic Sites) ameongeza.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi kutembelea banda la TAWA ili kupata maelezo ya fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi hiyo.

"Kama kauli mbiu ya Maonesho haya inavyosema kuwa Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji, nitumie fursa hii kuwaambia watanzania wote kuwa TAWA ni taasisi sahihi kwa biashara na uwekezaji kwani inatoa fursa za uwekezaji wa aina mbalimbali kama vile ujenzi wa loji, kumbi za mikutano katika maeneo yetu, kambi za watalii, michezo ya watoto.



No comments