Header Ads

ad

Breaking News

RAIS SAMIA MGENI RASMI KIKAO KAZI CHA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA, Ma-CEO, WAKURUGENZI WA BODI ARUSHA


Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu akizungumza na wahariri na waandishi wa habari Julai 15,2024 jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu amesema kuwa, Kikao Kazi cha Ofisi ya Msajili wa Hazina na maofisa watendaji wakuu, wakurugenzi na wenyeviti wa Bodi wa Taasisi za Umma, lengo lake kuu litakuwa dhana moja muhimu ya kuimarisha utendaji kazi wa makampuni ya Tanzania nje ya mipaka yetu.

Kikao Kazi hicho cha siku tatu kinachotarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 600, kitafanyika Agosti jijijni Arusha, huku Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi, kitakuwa na lengo la kuangalia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa mwaka jana aliposhiriki kikao kazi cha kwanza kama hicho.

Akizungumza na wahariri na waandishi kutoka vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina amesema lengo ni kuangalia uwekezaji na utoaji huduma wa taasisi za ndani nje ya mipaka, itaanza na taasisi zenye utayari, hqsa zilizopata mafanikio ndani ya nchi.

Msajili wa Hazina amesema kuwa, Rais Samia alikubali kuwa mgeni rasmi, kama walivyomwomba Siku ya Gawio, ambapo atashiriki kikao kitachojumuisha maafisa watendaji wakuu, wakurugenzi na wenyeviti wa bodi zaidi ya 600, kitajielekeza katika kuona makampuni ya Tanzania yanavyoimarisha shughuli zake nje ya mipaka yetu.

Amesema hayo yalikuwa ni maagizo na changamoto kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia mwenyewe aliyowapatia katika kikao cha kwanza kama hicho mwaka jana.

Mchechu amesema kwamba, katika dhima hiyo ya kutaka kuwa na uwekezaji wa taasisi za umma nje ya nchi, lengo lao ni kuanza na taasisi zenye utayari wa kuvuka mipaka ya nchi, huku lengo la pili likiwa ni kuzifanya taasisi zijue kwamba zinapaswa kubadilika, lakini zifanye hivyo zikiwa na taswira kubwa wanayoiona mbele.

Msajili wa Hazina ametoa mfano wa mashirika kama ATCL,  ambapo amesema pamoja na kutambulika kuwa, huduma zake zinapatikana nje ya nchi, lakini ofisi yake inafikiria kwamba zinapaswa ziende nje na kugusa jamii huko kwa ufanisi na ushindani mkubwa.

Ameongeza kuwa, Shirika la ReliTanzania (TRC) na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), ni kampuni ambazo lazima ziguse usafirishaji unaovuka mipaka ya nchi yetu na kwa kufanya hivyo, wataweza kupata mrejesho kama nchi, je wanaweza kupata maslahi ya kile walichokiwekeza huko. 

Mchechu amesema ndiyo maana wakenya, wananufaika na uwepo wa matawi ya benki zao za KCB na Equity ambazo zipo nchini, hivyo nirahisi kwa m kufanya biashara kwa ufanisi nchini na kwamba, Tanzania inapaswa kuwa mahiri, lakini ianze katika ngazi hizo.

Aliongeza kuwa, pamoja na hayo kikao hicho kina umuhimu mkubwa, ikiwemo kujua maagizo na maelekezo ya Serikali kupitia viongozi wakuu ya wapi wanataka tuelekee na kwa kasi gani, ikiwa ni pamoja na maafisa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi kubadilishana mawazo na mbinu mbalimbali za uendeshaji biashara.

Mchehu amesema katika 4R’s alizokuwanazo Rais Samia, Ofisi ya Msajili imechukuwa R mbili za ‘Reforms na Rebulding’ ambazo wataendelea kuzisimamia na kwamba, mabadiliko ya utendaji wa taasisi ni safari ndefu, na si jambo la siku mmoja, mwaka mmoja wala sio la taasisi moja.




No comments