Header Ads

ad

Breaking News

MSAMA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, akiitazama Tuzo ya Heshima aliyotukiwa na Clouds Media Julai 20,2024 jijini Dar es Salaam


Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Msama Promotions, Alex Msama, ametunikiwa Tuzo ya Heshima ya kutambua mchango wake mkubwa wa kuwa mwanzilishi wa kipindi cha muziki wa injili (Gospel), katika kituo cha Clouds FM Juni 20,2024 jijini Dar es Salaam.

Msama ambaye amekuwa chachu ya muziki wa injili nchini, kwa kuandaa tamasha kubwa la Pasaka lililokuwa likifanyika kila mwaka nchi nzima ambalo liliwaibua waimbaji wengi wa muziki huo,a mabo hivi sasa wanafanya vizuri sana.

Wasanii wengi nchini wamepita kwenye mikono ya Msama aliyeufanya muziki wa injili kujulikana na kupendwa zaidi ndani na nje ya Tanzania.

Tuzo hiyo ya Heshima iliyotolewa na Clouds FM, imeonesha jinsi wanavyothamini waanzilishi wa kipindi cha muziki wa injili ambapo hivi sasa unasikika kila mahali.

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, akipokea Tuzo ya Heshima aliyotukiwa na Clouds Media Group

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, akipokea Tuzo ya Heshima

No comments