Header Ads

ad

Breaking News

MSAJILI WA HAZINA ATAKA MASHIRIKA, TAASISI ZA UMMA KUWEKEZA NJE YA NCHI

 

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu akiwaeleza jambo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

VIONGOZI wa taasisi na mashirika ya umma wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa pili wenye kaulimbiu 'Mikakati ya Mashirika na Taasisi za Umma Kuwekeza Nje ya Tanzania' utakaofanyika hivi Agosti mwaka huu jijini Arusha.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, ametoa kauli hiyo leo Julai 15,2024 jijini Dar es Salaam, alipozungumza na wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu kikao chao CEOs Forum cha pili.

Amesema kikao cha kwanza kati ya viongozi wa taasi na mashirika ya umma kilifanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC),  Agosti 19 hadi 21, 2023 jijini Arusha.

Ameongeza kuwa, amesema viongozi ni kundi muhimu sana, pia kikao ni muhimu sana, kwani katika kikao hujumuika pamoja wenyeviti na ma -CEOs zaidi ya 600.

Amesema kaulimbiu hiyo inalenga kuhimiza taasisi na mashirika ya umma kuangalia zaidi fursa za kuwekeza au kupanua wigo wa huduma nje ya Tanzania. 

"Kaulimbiu hii inaunga mkono maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hasan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa wakati wa kikao Kazi cha mwaka 2023. Katika Kikao hicho, Mhe. Rais alielekeza kuangalia uwezekano wa Taasisi na Mashirika kufanya biashara au kupelekea huduma zake nje ya Tanzania."

Msajili wa Hazina amesema hiyo ni changamoto ambayo Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan aliwapa wakati alipofungua mkutano wao wa kwanza mwaka jana.Kikao kazi cha mwaka huu kitafunguliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Mchechu amesema Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia Taasisi na Mashirika ya Umma 309, ambapo idadi hiyo inajumuisha kampuni 56 ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache.

 "Taasisi na mashirika haya yamekuwa na mchango muhimu katika kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali zikiwemo sekta za fedha, elimu, afya, hifadhi ya jamii, viwanda, biashara na kilimo," amesema Msajili wa Hazina.

Ameongeza kuwa, taasisi hizo zinachangia kukuza Pato la Taifa, kuchangia mapato katika Mfuko Mkuu wa Serikali, kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kukuza ajira, kurahisisha upatikanaji wa huduma na bidhaa na kuhakikisha kuwa, huduma na bidhaa zinazotolewa zinakuwa na ubora na bei stahiki.

Hata hivyo, Msajili wa Hazina amesema kuwa, mchango wa mashirika na taasisi katika uchumi unaweza kuwa bora zaidi ya ilivyo sasa, lakini mashirika hayo yanatakiwa kujitathmini na kuboresha utendaji kazi ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea nchini, kanda na duniani.

Amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhamasisha ushirikiano na mageuzi ya kiuchumi kwa njia ya amani na maridhiano kupitia falsafa ya 4Rs; Reconciliation, Resilience, Reforms & Rebuilding. 

Mchechu amesema kwamba, Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo, wameendelea kujikita zaidi katika kufanyia kazi R mbili za mwisho yaani Reforms & Rebuilding ili kuhakikisha kuwa,  maono ya Serikali yanatekelezwa kikamilifu.

Msajili wa Hazina amesema baadhi ya maboresho yaliyofanyika na yanayoendelea kuimarisha usimamizi na utendaji kazi wa Taasisi na Mashirika ya Umma ni pamoja na kusomwa bungeni kwa Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma wenye mapendekezo muhimu ikiwemo wajumbe wa bodi kupatikana kwa njia ya ushindani.

Nyingine ni kuongezeka kwa tija ya uwekezaji wa Serikali katika kampuni ambazo inaumiliki wa hisa chache, kupewa uhuru wa kujiendesha kwa taasisi za kibiashara na za kimkakati na kuunganishwa na au kufutwa kwa baadhi ya taasisi ili kuongeza ufanisi. 

Amesema Ofisa Msajili wa Hazina  inalenga kuimarisha zaidi ufuatiliaji na tathmini ya mashirika ya umma, kukuza matumizi ya TEHAMA katika usimamizi wa Taasisi na Mashirika na kukuza ushiriki wa Sekta binafsi katika utekelezaji wa majukumu ya baadhi ya Taasisi na Mashirika ili kuongeza ufanisi.

Msajili wa Hazina amesema kuwa, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeona umuhimu wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu kushirikishwa kikamilifu katika kila hatua ya maboresho hayo ili kupata uelewa wa pamoja na hatua za kuchukua ili kufikia lengo linalotarajiwa na Serikali. 

Amesema upitia jukwaa hilo, viongozi, wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi watapitishwa katika maboresho yaliyofanyika, yanayoendelea na mipango ya baadaye ili kujua wajibu wao katika kuongeza ufanisi na tija.

Ameongeza kwamba, kwa kuwa malengo ni kuona Taasisi na Mashirika ya Umma yanajielekeza katika uwekezaji nje ya nchi, kikao kazi chao kwa mwaka huu kitajielekeza katika kupata uzoefu kutoka kwa mashirika ya ndani, lakini pia ya kimataifa yaliyofanikiwa katika nyanja mbalimbali.

Amesema maeneo muhimu yatakayofanyiwa kazi katika kikao kazi cha pili ni kujadili hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kikao kazi cha mwaka 2023 na Working sessions, kujadili fursa za kikanda na kimataifa kwa ajili ya Taasisi na Mashirika kuwekeza nje ya nchi.

Mengine ni kujadili na kupata uzoefu wa kiutendaji kutoka kwa wataalam wa ndani na nje ya nchi waliofanikiwa kiutendaji tukiangazia nchi za Singapore, China, UAE na Afrika Kusini,na namna bora ya kuboresha mitaji ya mashirika ili kuleta ufanisi wa kiutendaji na kuongeza ushindani.

Ameongeza kuwa, kubadilisha mitazamo na kuzifanya taasisi na mashirika yetu kuwa vichocheo vya maendeleo ya kiuchumi, watatapitia kwa pamoja na kukumbushana kuhusu mambo mengine muhimu ambayo wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wanapaswa kuzingatia katika usimamizi wa utendaji kazi ikiwemo miongozo mbalimbali ya Uendeshaji wa Mashirika ya Umma pamoja na umuhimu wake katika kutekeleza malengo ya Serikali kwa ufanisi.



Pia, watajadli changamoto mbalimbali za kiuendeshaji katika Taasisi pamoja na kuainisha mikakati ya kukabiliana nazo na Taasisi zilizofanya vizuri katika nyanja mbalimbali za utendaji kazi kama vile kutengeneza faida na kufanya mageuzi ya utendaji na hivyo kuboresha utoaji wa huduma zitatambuliwa na kupewa tuzo.



Mchechu amesema kuwa, matokeo yanayotarajiwa baada ya kikao kazi hicho ni Taasisi kujielekeza katika uwekezaji wa nje ya nchi na kuona Taasisi zikiendeshwa kwa ufanisi, zile zinazofanya biashara zitaongeza faida na hivyo kutoa gawio kwa mujibu wa sheria.


Mengine ni pamoja na taasisi ambazo zilianzishwa kwa misingi ya kutoa huduma zitaongeza uwezo wa kujitegemea katika uendeshaji wake  na

kuendelea kuwepo kwa mfumo endelevu wa kuzitambua taasisi zinazofanya vizuri na kuchukua hatua stahiki kwa taasisi ambazo hazifanyi vizuri.

Amesema katika Kikao Kazi cha mwaka huu, washiriki watajisajili na kuthibitisha ushiriki wao kupitia mfumo wa Tehama kupitia www.ceosforum.tz inayopatikana katika tovuti yetu mahususi kwa kikao kazi hiki.



No comments