Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI atembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza mtaalamu wa kutumia
kifaa cha DOZEE kutoka Kampuni ya Sakaar Healthtech Limited Yusuph Abdallah
aliyekuwa akimuelezea namna kifaa maalumu kijulikanacho kwa jina la DOZEE
kinachotumika kufuatilia maendeleo ya mgonjwa anayetibiwa akiwa nyumbani
kinavyofanya kazi alipotembelea banda la Taasisi hiyo jana wakati wa Maonesho
ya Biashara ya kimataifa ya 48 yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba
barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza mtaalamu wa afya
kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipotembelea banda hilo wakati wa
maonesho ya biashara ya kimataifa ya 48 yanayoendelea katika viwanja vya
Sabasaba barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa huduma za afya mtandao
kutoka kampuni ya cloudscrip Beatrice Mmari akimuelekeza mfanyakazi wa BOT
Lameck Kakulu namna ya kujisajiri katika mtandao ili kupata huduma za afya
zinazotolewa na JKCI wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya 48
yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba barabara ya kilwa jijini Dar es
Salaam.
Wananchi waliotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho ya kimataifa ya 48 ya biashara ya Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Picha zote na JKCI
No comments