Header Ads

ad

Breaking News

Maelfu watumwa kuukabili moto wa nyika California

Wazimamoto wakipambana na kuuzima moto wa nyika katika jimbo la California nchini Marekani.

                                                                                              Picha: Tayfun Coskun/Anadolu/picture alliance

Maelfu ya wazimamoto wametumwa kwenda kuukabili moto wa nyika unaowaka katika jimbo lenye idadi kubwa ya watu nchini Marekani la California.

Moto huo ambao ndio mkubwa zaidi tangu kuanza kwa msimu wa kiangazi mwaka huu, umelazimisha maelfu ya watu kuhamishwa na tayari umesambaa na kuchoma eneo lenye ukubwa wa ekari 370,000. Ulizuka tangu jumatano iliyopita kaskazini mwa jimbo hilo umbali wa kiasi saa tatu kutoka mji mkubwa wa San Francisco.

Hata hivyo hadi sasa hakuna mtu aliyepoteza maisha kutokana na janga hilo. Hapo jana Idara ya maafa ya jimbo la California ilitangaza kukituma kikosi cha wazimamoto 4,900, helikopta 33, magari zaidi ya 400 na ndege kadhaa kupambana na moto huo.

Taarifa zinasema asilimia 12 ya moto huo tayari umedhibitiwa na kupungua kwa kiwango kumeleta matumaini ya kuuzima kikamilifu.            (DW)

No comments