Header Ads

ad

Breaking News

KIKWETE: RAIS SAMIA AMEKAMILISHA MRADI WA SGR, LICHA YA KUUPOKEA KATIKA HATUA ZA MWANZO

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesema tumpongeze Rais Samia kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, huku vipande vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Akijibu swali la Idriss Sultan katika Podcast maalumu iliyofanyika nyumbani kwake, Rais huyo wa Awamu ya Nne wa Tanzania, amesema kuwa wazo la SGR lilianza baada ya Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa kufanya mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda juu ya kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Kigali.

Hata hivyo, Kikwete amesema tumpongeze Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi huo utakaogharimu takriban dola bilioni 7 za kimarekani.

No comments