INEC KUZINDUA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA MPIRA KURA KIGOMA JULAI 20
Mkali wa Singeli Abdallah Ahmed m Inbox Frank Balile
9:47 AM (1 hour ago) to me
Mkali wa Singeli Abdallah Ahmed maarufu Dulla Makabila akiwa jukwaani kutumbuiza katika tamasha hilo
la burudani kuelekea uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura mkoani Kigoma.
Katika Tamasha hilo kundi la Waobama waliibuka washindi katika vikundi vya kucheza dansi vilivyokuwa vikishindanishwa na kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na Singeli, Sande
Mangu almaarufu Linex na Abdallah Ahmed maarufu Dulla Makabila leo Julai 18,2024 wameingiza shangwe
kwa wakazi wa Kigoma kwa kutoa burudani kali katika Tamasha
la uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura.
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inataraji kuzindua uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Julai 20,
2024 utakaofanyika katika Uwanja wa Kawawa ulipo Ujiji
Kigoma na mgeni rasmi akifaraji kuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Majaliwa Kassim
Majaliwa.
Wasanii hao waliopanda jukwaani kwa nyakati tofauti
kutumbuiza katika tamasha hilo maalum kuelekea uzinduzi
wa Ubereshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
lililokwenda sanjari na utoaji wa Elimu ya Mpiga Kuru
kuhusu Uboreshaji wa Daftari.
Alianza kupanda jukwaani Linex ambaye ni mzaliwa wa
Kigoma na ambaye alikuwa uwanja wa nyumbani akiimba
baadhi ya nyimbo zake maarufu ukiwepo wimbo maalum wa
kuhamasisha watu kujitokeza kuboresha taarifa zao na
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura.
Linex anae tamba kwa sasa na kibao chake cha 'Mahama ya Mapenzi' kabla ya kushika jukwaani alitumbuiza kwa wimbo
maarufu aliyeyoimba na wasnii wenzake kutoka Kigoma
wa 'Leka dutigite' aliyoimba na kundi
lao la Kigoma All Stars akiwa na wasanii wenzake kutoka Kigoma ambao ni Abdu Kiba, Baba
Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond, Linex, Makomando,
Mwasiti, Ommy Dimpoz, Queen Darling, Rachel na mwanasiasa
maarufu mzaliwa wa Kigoma Zitto Kabwe.
Makabila yeye nae aliimba nyimbo zake kadhaa ikiwepo
'Pita Huku', 'Furahi', 'Hujaulamba', lakini bila kusahau
nyimbo za Simba na Yanga ambazo ziliibua shjangwe kubwa
jukwaani.
Makabila atatumbuiza tena siku ya Uzinduzi Julai
20,2024 mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa.
Wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Kawawa
Kigoma Ujiji walionesha kufurahishwa na burudani hiyo
iliyokonga nyoyo zao vilivyo.
Aidha, Mbali na Dulla Makabila na Sande Linex pia
vikundi mbalimbali vya burudani kama Warumba Shauri,
Smart Boys , Vijana Rumba, Chama Dansa, Mwandiga One,
Waobama.
Katika Tamasha hilo kundi la Waobama waliibuka washindi
katika vikundi vya kucheza dansi vilivyokuwa
vikishindanishwa na kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa
Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness
Aswile.
Vikundi mbalimbali vilivyokuwa vikishindana katika
tamasha hilo, vikitoa burudani.
Katika Tamasha hilo kundi la Waobama waliibuka washindi katika vikundi vya kucheza dansi vilivyokuwa vikishindanishwa na kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile.
No comments