Header Ads

ad

Breaking News

Hospitali ya JK yaendesha kliniki, yatoa ushauri magonjwa yasiyoambukiza

Katibu Afya Hospitali ya JK, Marietha Mashimba Mboje

Na Mwandishi Wetu

HOSPITALI ya JK iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, imeendesha kliniki ya matibabu kwa watoto na kina mama iliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali hiyo Mikadi wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa kliniki hiyo, Katibu Afya Hospitali ya JK, Marietha Mashimba Mboje aliwapongeza wananchi waliojitokeza kupata vipimo na matibabu yaliyofanywa na madaktari bingwa wa hospitali hiyo.

Mboje alisema kuwa, matibabu hayo yalifanywa na daktari bingwa wa watoto aliyesimamia matibabu ya watoto na kutoa elimu ya afya kwa wananchi waliojitokeza kupata matibabu hayo.

"Kwa upande wa watoto, tulikuwa na daktari bingwa ambaye alisimamia kila kitu kinachohusu afya ya watoto, ikiwemo kutoa elimu ya afya kwa wananchi," alisema Katibu huyo.

Aliongeza kuwa, mbali na daktari bingwa wa watoto, pia walikuwa na daktari bingwa wa wanawake ambaye aliwafanyia uchunguzi na kuwapa tiba kina mama waliojitokeza kwenye kliniki hiyo.

 Katibu Afya huyo alisema kuwa, watalaamu wa hospitali hiyo walitoa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza ambapo aliwataka wananchi hao kuzingatia vyakula wanavyokula.

Alisema ni muhimu kwa wananchi kujua wanakula nini, kwa wakati gani, kwani huambukizwa zaidi kutokana na mtindo wa maisha, hivyo aliwataka kuwaona wataalam wa lishe ambao walikuwepo kwenye viwanja hivyo.

"Tukibadilisha mtindo wa maisha, ni rahisi zaidi kujikinga na kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza," amesema Katibu Afya Hospitali ya JK.

Mboje alisema kuwa, Hospitali ya JK hutoa hutuma za kibingwa ikiwa na madaktari bingwa wa magonjwa ya tezi dume, wanawake, magonjwa ya ndani, watoto na mifupa, huku akisisitiza kuwa, wajawazito hupata huduma maalum hadi watakapojifungua.

Alisema huduma zao hazina gharama kubwa, hivyo amewataka wakati wa Kigamboni na maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam, kwenda kupata matibabu katika hospitali hiyo yenye vifaa vya kisasa.

Mboje alizitaja huduma nyingine zinazotolewa na Hospitali ya JK ni kuonana na daktari (OPD), kulazwa, huduma za dharura (emergency), uzazi na kujifungua (labor), maabara (laboratory), duka la dawa (pharmacy), afya ya uzazi (RCH) na kliniki za madaktari bingwa.

Nyingine ni magonjwa ya wanawaek (gynaecology), mfumo wa mkojo (urology), magonjwa ya ndani (physian), pua, sikio na koo (ENT), mifupa (orthopedic), upasuaji (surgery), daktari bingwa wa watoto (pediatric) na magonjwa ya moyo (cardiac).

Pia, alisema Hospitali ya JK inapokea wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ya NHIF (supplementary), Assemble, Jubilee na wanaolipa moja kwa moja (cash).




No comments