Header Ads

ad

Breaking News

DKT.ABBASI AVUTIWA NA MAONESHO KIDIJITALI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hassan Abbasi (kushoto), akiangalia vitu mbalimbali alipotembelea banda la Makumbusho ya Taifa la Tanzania lililopo ndani ya Banda kubwa la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam 

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hassan Abbasi amesema amevutiwa na namna ambavyo Makumbusho ya Taifa la Tanzania inavyotumia mifumo ya kidijitali kuonesha taarifa mbalimbali kuhusu Urithi wa Asili na Utamaduni wa Tanzania.

Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo, Julai  2,2024 alipotembelea banda la Makumbusho ya Taifa la Tanzania lililopo ndani ya Banda kubwa la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kuweka maonesho kwa njia ya kidijitali kutawawezesha watalii wengi wa ndani na nje ya nchi kujifunza kwa urahisi, na kutamani kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii wa wanyama pori na Malikale vinavyopatikana nchini Tanzania.

Dkt.Abbasi ameongeza kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha idadi ya watalii wanaotembelea vivutio mbalimbali inaongezeka maradufu, kwa kuongeza wigo wa utalii kwenye sekta ya utamaduni na misitu badala ya kujikita kwenye utalii wa wanyama pori pekee.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hassan Abbasi (kushoto)

No comments